Mafunzo ya Mfumo mpya wa kutengenezea bajeti (PLANREP) na wa kutolea taarifa za kifedha kutoka katika ngazi za msingi za kutolea huduma (FFARS) yamefikia siku ya nne tangu yalipoanza hapo siku ya Jumatatu hapa Wilayani katika ukumbi mdogo wa Mikutano. Mafunzo yanaendelea vema na washiriki wanaonyesha umoja na ushirikiano mzuri mda wote wa mafunzo. Wamekuwa wakiuliza maswali mbalimbali kwa wawezeshaji na kubaini changamoto ambazo baadhi ziliwasilishwa jana tarehe 20/9/2017 kwa wasimamizi kutoka TAMISEMI. Akiongea siku ya jana Bw. Elisa kutoka TAMISEMI alisema kutokana na changamotmo zilizokuwepo awali ndizo zilizopelekea kuanzishwa mfumo mpya unaotumia mtandao na uliorahisi kwa kufanyiwa maboresho na kila mmoja anayetumia kupata maboresho pindi tu aingiapo kwenye mfumo.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.