Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amesema serikali ya Wilaya kwa kushirikiana na wananchi imepata mafanikio mengi ambayo inajivunia nayo kutokana na jitihada kubwa zilizofanywa na serikali za awamu ya kwanza, pili, tatu, nne tano na ya sita
Kwa kutoa mchango mkubwa ambapo wananchi walishiriki kikamilifu kuunga mkono jitihada zilizofanywa na waasisi wa Muungano wa Tanzania. Mkuu wa Wilaya amesema
"Kuwepo kwa Muungano huu ni kuwepo kwa mahusiano ya karibu na ya kihistoria baina ya Tanganyika na Zanzibar katika nyanja mbalimbali kama vile udugu wa damu, biashara, utamaduni, lugha na mahusiano ya karibu kisiasa hususani vyama vya TANU na ASP."
Mkuu wa Wilaya amesema hayo katika kongamano la Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanzania lililofanyika katika ukumbi wa HalmashaurI ya Wilaya ya Maswa Tarehe 26 April 2024.
Mhe Kaminyoge amebainisha kuwa wadau wa maendeleo waliopo ndani na nje ya Wilaya zikiwemo Asasi mbalimbali (madhehebu ya dini, mashirika yasiyo ya kiserikali wamechangia katika sekta mbalimbali za uzalishaji mali, huduma za kijamii utawala Bora na ulinzi na usalama ili kuongeza tija na kuleta mafanikio.
Mkuu wa Wilaya amesema serikali imeendelea kuboresha sekta ya Elimu kwa kutoa Elimu bila malipo ambapo bilioni 2.8 hutolewa Kila mwaka kwa ajili ya Elimu msingi na Elimu Sekondari ikiwa Elimu msingi inapata shs bilioni 1.2 na Elimu Sekondari inapata shs bilioni 1.6
Pia shule za msingi zimeongezeka kutoka shule 27 mwaka 1964 mpaka kufika shule 135 za serikali na binafsi 3 vivyo hivyo Elimu Sekondari haikuwa na shule ya Sekondari na kidato Cha sita lakini Sasa Kuna shule 44 za serikali na 2 za binafsi na shule za kidacho Cha sita 3
Huduma ya afya pia zimeboreshwa sana ambapo vituo vya kutolea huduma za Afya vimeendelea kujengwa na kukamilishwa pamoja na vilivyojengwa kwa nguvu ya wananchi ambapo katika wilaya ya Maswa jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 56, Hospitali 1, Vituo vya Afya 4 Zahanati 48 za serikali na Zahanati 3 za binafsi
Lengo la serikali ni kuhakikisha huduma hizo zinasogea karibu na wananchi ambapo serikali imeendelea kutoa Fedha zaidi yailioni 600 kwa ajili ya vifaa tiba na dawa ili wananchi wasipate shida.
Katika sekta ya barabara Wilaya ya Maswa imeendelea kupiga hatua kubwa kwa kufungua barabara ambapo jumla ya kilometa 1084.2 zinapitika ikiwa lami kilometa 4.78, changarawe 499.27 na udongo kilometa 580.15.
Katika mwaka wa Fedha 2022/2024 Wilaya ya Maswa imeendelea kuimalisha miundombinu ya barabara, madaraja na vivuko vyenye thamani ya shs bilioni 4 na pia Mhe Rais ametoa shs milioni 100 kwa ajili ya kuirudisha miundombinu ya barabara iliyoharibika katika kipindi Cha mvua jumla ya km 16 za mjini, Lalago na Malampaka kufanyiwa malekebisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.