Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wameipongeza serikali kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo
Hayo yalibainishwa katika kikao Cha robo ya tatu ya mwaka kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Maswa leo tarehe 12 Mei 2022.
Katibu wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ndg. Simon S. Berege amesema serikali imetoa shs bilioni 12,132,146,392.39 kwa ajili ya miradi mbalimbali katika wilaya yote ya Maswa fedha hizo zitaweza kukamilisha miradi yote ambayo haijakamilika.
Pia ndg Berege ametumia kikao hicho kwa kuwapongeza watumishi wote na waheshimiwa madiwani kwa kumaliza vizuri robo hiyo na kuwa nafasi ya 27 kitaifa, na kwenye mradi wa EP4R unaotekelezwa na Waingereza, Maswa imekuwa nafasi ya pili kitaifa kwa kufanya vizuri.
Akitoa salamu za serikali Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amempongeza Mhe. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kutoka serikali kuu kwa asilimia 100%, ili ziweze kutumika katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri ya Maswa ikiwemo Afya, Maji, Barabara, Elimu na sekta nyingine
Pia Mhe Mkuu wa Wilaya amewashukuru waheshimiwa Madiwani, Mkurugenzi na wataalamu kwa usimamizi mzuri wa mapato ya fedha zilizotengwa kwenye 40% inayotokana na mapato ya ndani ili iweze kupelekwa kwenye miradi kwa ajili ya kukamilisha na kuzinduliwa katika mwenge wa uhuru. Pamoja na 10% ya fedha zinazokwenda kwa vijana na wanawake zitolewe kwa 100% ili kukuza mapato ya vikundi.
Mkuu wa Wilaya amewasisitiza waheshimiwa Madiwani na watendaji kutoa elimu juu ya umuhimu wa sensa ya watu na makazi katika jamii kupitia vikao mbalimbali ambavyo vitafanyika katika maeneo yao na agenda kubwa katika vikao hivyo iwe ni zoezi la sensa litakalofanyika Augusti 23, 2022.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji ambaye alikuwa Katibu wa kikao hicho amewaeleza wajumbe kuwa changamoto zilizojitokeza amezichukua na ataenda kuzifanyia kazi na wataalamu wake ili kuhakikisha mipango yote ya maendeleo inakamilika kwa ubora wa hali ya juu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.