Madiwani wa Manispaa ya Moshi wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Mhe. Stuart Nkinda na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi ndg. Rashid Gembe wamefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu yenye lengo la kubadilishana uzoefu na kujifunza namna ambavyo Halmashauri ya Maswa imeweza kumiliki Kampuni ambayo inaiingizia mapato Halmashauri.
Waheshimiwa madiwani wa manispaa hiyo wameambatana na Mstahiki Meya wa Manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa, na baadhi ya wataalamu kutoka Manispaa hiyo ya Moshi leo tarehe 26 May 2022.
Wakiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa waheshimiwa madiwani, Mstahiki Meya, Mkurugenzi na wataalamu kutoka Manispaa ya Moshi wametembelea viwanda mbalimbali vya Kampuni ya Ng'hami ambavyo ni Kiwanda Cha Unga wa Viazi lishe kilichopo Kata ya isanga Kijiji cha Njiapanda, Duka la dawa lililopo Kata ya Sola Kitongoji cha Mwashigela, Kiwanda cha Ngozi kilichopo Kata ya Binza Kitongoji cha Ujenzi, Kiwanda cha kupanga madaraja ya Mchele Kata ya Malampaka Kijiji cha Malampaka, Kiwanda cha Chaki na vifungashio kilichopo Kata ya Nyalikungu Kijiji cha Ng'hami na Kiwanda kinachomilikiwa na kikundi jumushi cha Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu Kiwanda cha Mikate kilichopo Kata ya Nyalikungu Kijiji cha Ng'hami kuona jinsi uzalishaji unavyofanyika
"Nawapongeza Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na kuwashukuru watendaji wote wa Kampuni kwa project mbalimbali wanazozifanya Miradi ya ngazi ndogo, ya kati na ngazi kubwa kabisa ni jambo zuri kwa sababu hata kwenye maisha tuna maendeleo kwa ngazi tofauti tofauti kwa hiyo tutaweza kuanza " amesema Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi.
Naye Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Ng'hami Ndg. Levocatus Bunduki amewasihi waheshimiwa Madiwani pamoja na Mkurugenzi na wataalamu kutoka Manispaa ya Moshi wanapotaka kuanzisha Kampuni ni lazima wachague mtu amabaye ni mwaminifu na anayejitoa katika kazi yake kwa usimamizi ili Kampuni hiyo iweze kuendelea.
"Mkurugenzi, Mstahiki Meya mnapochagua watu kule chagua mtu mwenye "DNA" ya kuangalia malifedha na malivitu" Bunduki amesema.
Nae Ndg. Magembe meneja uzalishaji wa Kampuni ya Ng'hami amesema kuwa Kampuni hiyo ilianza mwaka 2019 na mpaka sasa inazalisha bidhaa mbalimbali ikiwepo Unga wa viazi lishe wa aina mbalimbali , Mchele , pamoja na kutoa huduma ya dawa kwa wahitaji na mpaka sasa kampuni ina watumishi 17 walioajaliwa,vibarua 22 wa mikataba ya muda mfupi ambao wanafanya kazi katika maeneo tofauti tofauti ya viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani na ushindani katika biashara.
Nae Afisa mipango daraja la pili Ndg. Ntobi Ntambi kutoka Ofisi ya Mipango Wilaya ya Maswa amesema Kampuni imejipanga vizuri kwa kuwa kampuni ilipata fedha bilioni 8.2 zilizotolewa kwenye bajeti ya mwaka 2018/2019 kwa ajili ya viwanda viwili vya Chaki na Vifungashio ambapo mpaka sasa mitambo inaendelea kufungwa katika Kiwanda cha Chaki ambacho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha katoni 90 kwa siku za Chaki. Pia kampuni imeweza kutoa gawio la shs milioni 10 kwa wanahisa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.