• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Lishe bora ni mwanzo wa mafanikio ya wanafunzi kuelewa darasani: Ndg Gyunda

Posted on: October 30th, 2023

Afisa lishe wa Wilaya ya Maswa Ndg Abel Gyunda amewataka vijana wa rika balehe kutumia  mlo kamili unaohusisha makundi matano ya chakula lengo likiwa ni kumsaidia mwanafunzi  kuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa darasani pamoja na kukua vizuri kimwili, kiafya na kisaikolojia ili kuepukana na udumavu, uzito kupita kiasi pamoja na ukondefu.

Ndg Gyunda ameyasema hayo katika maazimisho ya siku ya lishe duniani ambayo kiwilaya yamefanyika  katika shule ya sekondari ya wasichana Maswa leo tarehe 30/10/2023 wakati akitoa Elimu ya namna bora ya kula mlo kamili kwa wanafunzi wa lika la vijana balehe ambapo wanafunzi pamoja na walimu walishiriki katika maadhimisho hayo.

Lengo la maadhimisho hayo ni kujenga uelewa kwa jamii juu ya umuhimu wa lishe bora kwa vijana balehe na kuhamasisha sekta mbalimbali kuweka kipaumbele katika masuala ya lishe hasahasa kwa vijana kuanzia miaka 10-19.

Aidha amesema katika rika la vijana balehe  ongezeko la virutubishi mwilini huongezeka kutokana na viungo vyao kukua hivyo ametoa ushauri kwa kundi hilo kutumia  lishe bora ili kukabiliana na mabadiliko hayo.

Afisa lishe ametoa wito kwa vijana balehe kuepuka kula vyakula vyenye sukari nyingi, matumizi ya vileo, chumvi nyingi, na mafuta mengi kwa sababu ni hatarishi kwa lishe katika rika hilo hivyo vijana hao wanatakiwa kupata kirutubishi cha madini chuma ambayo ni muhimu sana katika kuongeza wingi wa damu mwilini.

Ameongeza kuwa vijana hao wanatakiwa kujishughulisha kwa kufanya kazi na sio kukaa tu bila kazi lengo likiwa ni kupunguza lishe duni katika kundi hilo ambalo kwa kiasi kikubwa linapata athari ya kupungua kwa nguvu kazi kwa kutokufanya maamuzi ya busara pamoja na udumavu kutokana na viungo kutokuwa  sawasawa ambapo husababisha magonjwa sugu yasiyo ya kuambukizwa ambayo ni kisukari, saratani na shinikizo la damu.

Maadhimisho hayo yameenda sambamba na tahmini ya hali ya lishe kwa kupima  urefu pamoja na uzito kwa kundi hilo la rika la vijana balehe ambapo tahmini imeonyesha kundi hilo linazingatia lishe bora na pia amewaomba waendelee kutumia vyakula hivyo kwa wingi ili kuepukana na udumavu.

Matangazo

  • TANGAZO LA UHAMASISHAJI CHANJO YA MIFUGO January 21, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MASWA

    March 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.