Kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini (CAMARTEC) ni kitovu cha teknolojia ya kihandisi vijijini taasisi hiyo ipo chini ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Katika Wilaya ya Maswa taasisi hiyo imeanzisha kituo na kitovu cha Teknolojia za kihandisi katika kijiji cha Mwandete Kata ya Sangamwalugesha.
Kituo hicho kinatoa huduma za mafunzo ya teknolojia mpya katika zana za kilimo, matumizi ya gesi itokanayo na vinyesi vya wanyama ( BIOGAS), uuzaji, ukodishaji, matengenezo ya zana hizo na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu matumizi ya zana na teknolojia hizo kwa wakulima wote wa Wilaya ya Maswa na nje ya Maswa.
Zana zinazopatikana katika kituo hicho ni Trekta zilizoundwa na taasisi hiyo, Matela ya kubebea mizigo yanayokokotwa na wanyama (Animal drawn carts), mashine za kupandia mazao mbalimbali kwa kutumia wanyamakazi (Mechanical planters), vifaa vinavyotumia nishati ya jua kukaushia mbogamboga, viazi, matunda pamoja na vifa vya kuchemshia maji kwa kutumia mionzi ya jua ( Solar dryer and heaters).
Pia kuna mashine za kupura mazao mbalimbali kama mahindi, mtama, karanga, na alizeti ambazo zinatumia mafuta, (Threshing mashine), mashine za kutengeneza siagi ya karanga (Peanut butter mashine), mashine za kukatakata na kufunga nyasi kwa ajili ya chakula cha mifugo (Straw chopper and hay baler mashine).
Aidha kituo hicho kinatoa huduma ya uwekaji wa vifaa vya gesi asilia itokanayo na vinyesi vya wanyama kwa ajili ya matumizi ya nyumbani mfano kupikia (Biogas plant installation) pamoja na elimu kwa wakulima kuhusu matumizi ya zana hizo ili kurahisisha ufanisi wa shughuli za uzalishaji.
Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imetoa wito kwa wananchi wote kufika katika kituo hicho ili kujipatia zana, ushauri na kujifunza namna ya kutumia teknolojia mpya ya zana za kilimo.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.