Serikali imetoa kiasi chaTsh. 400,000,000/= kwa jili ya ujenzi wa kituo cha Afya katika kijiji cha Mwabayanda Kata ya Mawabayanda. WDC ya kata hiyo imepokea vema taarifa ya uwepo wa fedha hizo na kuahidi kushirikiana na Serikali ili kufanikisha ujenzi wa Kituo hicho.
Fedha hizo zinalenga kujenga miundo mbinu ifuatayo; Nyumba ya Mganga, Maabara, Jengo la upasuaji, Wodi ya akina mama na watoto na chumba cha kuhifadhia maiti. Aidha wajumbe wa WDC wamekubaliana kwa pamoja kupitia vijiji vyote 3 vinavyounda Kata hii kukamilisha jengo lililopo kwa kutumia nguvu za Wananchi ambayo ni kupitia mchango wa Tsh. 50,000/= kwa kila Kaya.
Kuonyesha kuwa wako tayari kesho watakuwa na Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mwandu, keshokutwa kijiji cha Ilamata na Mwabayanda ili kufikisha ujumbe wa ujenzi wa Kituo cha Afya na ushiriki wa wananchi katika ujenzi huo ili kazi zianze mara moja.
Pia kupitia kikao hicho wajumbe wamepewa taarifa ya kupokea Tsh. 150,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa nyumba sita 6 za Walimu katika shule ya Sekondari Mwabayanda ambao mkataba kwa ajili ya ujenzi tayari ushafungwa.
Katika kikao hicho maalum baadhi ya wajumbe wameanza kutoa michango yao ya fedha ili kufanikisha ujenzi ulio mbele yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.