Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Abdalla Shaib Kaim amesema kituo cha teknolojia za kihandisi kinatakiwa kuwajengea uwezo wananchi na uelewa kuhusu zana za Kilimo ili ziwaongezee kasi ya uzalishaji kwa kuongeza tija katika shughuli za Kilimo.
Mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2023 umezindua kitovu cha teknolojia za kihandisi Kijijini (CAMARTEC) kilichopo Kijiji cha Mwandete Kata ya Sangamwalugesha. Kituo hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha wakulima na wafugaji kupata huduma za teknolojia za kihandisi ikiwamo zana za Kilimo ufugaji na uvuvi ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya Kilimo.
Mradi huo unatekelezwa na wizara ya viwanda na biashara kupitia kituo cha zana za Kilimo pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Akisoma taarifa Afisa Rasilimali Watu Ndg. Boniface Chatila, Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu - CAMARTEC amesema kituo hicho kinatoa huduma mbalimbali kwa wananchi kwa kutoa mafunzo ambapo vijana na wanawake 50 wamepata mafunzo, ukodishaji wa zana hizo pamoja na uuzaji.
Nae Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za maendeleo ya kijamii Mhe. Stanslaus Nyongo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Fedha kwa ajili ya mradi huo ambao utasaidia wananchi wengi katika Kilimo.
Aidha amesema kuwa wananchi wakitumie vizuri kituo hicho kwa ajili ya kukodi zana hizo wakati wa kilimo na kupata ushauri ambao utawasaidia kuongeza tija kwa wakulima na wafugaji.
Afisa Utumishi CARMATEC akisoma taarifa kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge 2023
Msimamizi wa Kituo akitoa malezo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2023
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.