Waheshimiwa Madiwani Wilayani Maswa leo tarehe 24/8/2017 wamepewa semina kuhusu kilimo cha mkata hasa katika zao la Pamba.
Kilimo cha mkataba kinamaanisha uzalishaji wa mazao unaofanyika kwa wakulima kuingia makubaliano (mkataba) na wanunuzi wa mazao hayo. Hapo awali kimekuwa kikitumika tangu kuanza kwa kilimo cha pamba (Vyama vya Ushirika) hadi 1994.
Mkataba unaweka masharti ya namna ya kuzalisha na kuuza mazao hayo na kila upande huwa na majukumu ya kutekeleza.
Vipengele 3 muhimu vya mkataba:-
i) Upatikanaji wa soko
Mnunuzi na mkulima hukubaliana masharti ya kuuza na kununua zao
ii) Upatikanaji wa pembejeo
Mnunuzi huwa na jukumu la kutoa pembejeo zinazohitajika na wakati mwingine hugharamia kazi ya kuandaa shamba na ushauri wa kitaalam.
iii) Usimamizi Maalum
Mkulima hukubali kufuata taratibu za kitaalam zinazo shauriwa kwa matumizi ya pembejeo,mbinu bora za uzalishaji na uvunaji.
Kilimo kwa njia ya mkataba humlazimisha mnunuzi kujihusisha kwa karibu na uzalishaji wa pamba badala ya kununua na kuondoka.
Faida za kilimo cha mkataba kwa wakulima
i) Kupata pembejeo na huduma za Ugani
Utaratibu huu utawapa wakulima pembejeo na huduma nyingine kama kuwalimia kwa trakta na huduma za ugani.
ii) Upatikanaji wa mikopo
Ili kuondokana na tatizo la Wakulima kuwa na pembejeo za kutowatosheleza tunahitaji kutafakari ni jinsi gani mkulima ataongeza tija ambayo itamwezesha kusimamia.
mradi wake wa kilimo na kuufanya kuwa wa kibiashara.
iii) Matumizi ya Teknolojia Sahihi
Mbinu mpya za uzalishaji zinahitajika kuongeza kwa hali ya juu ubora wa mazao ya kilimo unaohitajika kwenye soko. Hivyo katika zao la pamba ni lazima huduma za ugani zitolewe baina ya Serikali na wanunuzi wa pamba.
iv) Utoaji wa Ujuzi (Stadi)
Ujuzi atakaopatiwa mkulima kupitia kilimo cha mkataba ni pamoja na matumizi sahihi ya viuadudu, matumizi bora ya raslimali,na umuhimu wa ubora wa pamba. Ujuzi na mbinu hizi mkulima huzitumia pia ktk kuzalisha mazao mengine ya biashara na chakula.
v) Kupata masoko ya uhakika
Wakulima wadogo wanatatizwa na kukosa fursa ya masoko kwa mazao wanayozalisha hivyo kuwawia vigumu kubadili na kulima mazao mengine.
Kilimo cha mkataba kinawapa sululuhisho la tatizo hili kwani uwahakikishia soko na kuwapa uhakika wanunuzi wa kupatikana kwa mali ghafi.
Faida ya kilimo cha Mkataba kwa wanunuzi wa pamba
i) Uzalishaji wa kuaminika
Kilimo cha mkataba ni njia ya kupata malighafi ya uhakika kuliko utaratibu wa kununua pamba katika masoko ya wazi.
ii) Ubora usiobadilika
Kilimo cha mkataba kwa kutumia vikundi vya wakulima kama wakala wa kununua pamba kinalenga kuongeza uwazi ktk magulio na hivyo kupandisha kiwango cha ubora wa pamba.
Aidha wamehimizwa kusimamia suala hili ili utekelezaji wake uweze kuleta ufanisi.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.