ataalam mbalimbali wilayani Maswa wamefanya kikao maalum kwa ajili ukasanyaji mapato hapa Wilayani. Katika kikao hiki wamepitishwa kwenye mambo muhimu ya utekelezaji mbalimbali zikiwemo sheria na taratibu zinazowaongoza katika kazi hiyo.
Wamejifunza Sheria kuu na sheria ndogo za mapato pamoja na kufundishwa jinsi ya kutumia mfumo wa kielektroniki kukusanya ushuru kwenye maeneo yao.
Baada ya kupitishwa katika masuala hayo yote, Mkurugenzi Mtendaji ametumia fursa hiyo kutoa maagizo kwa viongozi hao. Amesema kila Mtendaji wa kijiji kisicho makao makuu ya Kata kuanzia Jumatatu tarehe 3/2/2020 aanze kusaini katika kitabu cha mahudhurio cha shule iliyoko katika kijijichake na walioko makao makuu ya kata wasaini katika ofisi ya mtendaji wa Kata.
Pia Maafisa Ugani wote kuanzia Jumatatu 3/2/2020 waanze kusajiri Wakulima katika Daftari la Wakulima na kuweka taarifa za kuwatembelea na kutoa huduma kwa Wakulima na Wafugaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.