Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imeipongeza Halmashauri ya Maswa kwa usimamizi mzuri wa miradi, baada ya kamati hiyo kutembelea na kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri.
Kamati imetembelea miradi minne ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ambayo ni Ujenzi wa Kiwanda cha Chaki kilichopo Ng’hami Kata ya Nyalikungu, Mradi wa Josho katika Kijiji Cha Mwanhegele Kata ya Nyabubinza, Ujenzi wa Mnada wa Malampaka katika Kijiji cha Gulung’washi Kata ya Malampaka na Mradi wa Josho katika Kijiji cha Jija Kata ya Jija.
Ziara hii ya wajumbe imefanyika ikiwa ni ukaguzi wa utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira kuona namna ambavyo miradi inatekelezwa.
Kwa upande wao baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira wameipongeza Halmashauri kwa kusimamia vizuri miradi hiyo na kuwaomba waendelee kuitunza vizuri miundombinu hiyo kwa kuwa ni chachu ya maendeleo kwa wananchi na Halmashauri.
Aidha wataalamu wameihakikishia Kamati kuwa miradi yote inayoendelea kujengwa itakamilika kwa wakati tayari fedha na vifaa mbalimbali vimeletwa, lengo likiwa ni kumaliza miradi kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Kamati hiyo ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira imepokea baadhi ya changamoto zilizojitokeza katika baadhi ya miradi na kuahidi kuitafutia suluhisho, ili miradi iliyoanzishwa katika maeneo hayo isikwamishe maendeleo ya eneo husika kupata mapato pamoja na Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.