Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Maswa ikiongonzwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyonge leo tarehe 15 januari 2025 imepitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Kamati hiyo imepitisha Rasimu hiyo baada ya kupitia mapendekezo yaliyowasilishwa ambayo yamezingatia vipaumbele vya Halmashauri katika maeneo muhimu ambayo ni kuboresha miundombinu ya elimu, kukarabati miundombinu ya Afya, kuwezesha wananchi kwa kutoa fursa ya upatikanaji wa mikopo ya asilimia 10%.
Ujenzi wa soko la kisasa katika eneo la MADECO, pamoja na kusimamia uzalisha katika kiwanda cha chaki ili kiweze kutoa matokeo chanya pamoja na kuongeza tija ya uzalishaji katika sekta ya kilimo.
Akiwasilisha Rasimu ya Mpango wa Bajeti Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndugu, Julius Ikongola amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imekisia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni 47,231,857,280.00 ikiwa ni ongezeko la shilingi milioni 379,943,920.00 sawa na asilimia 0.81%. Ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2024/2025 ya kiasi cha shilingi bilioni 46,851,913,360.00.
Pia ndugu, Ikongola ameongeza kuwa ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa bajeti ya mapato ya ndani ya Halmashauri, Ruzuku ya mishahara pamoja na Ruzuku ya miradi ya maendeleo.
Pia kamati hiyo imetoa pongezi kwa Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya chini ya Mkurugezi Mtendaji kwa kuandaa bajeti nzuri ambayo ina vipaumbele vyote ambavyo vitaenda kujibu changamoto mbalimbali za wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.