Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Maswa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge imeanza ziara ya siku tatu yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya Elimu, Afya na Kilimo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo amesema maelekezo ya Mhe Wazari Mkuu kwa wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa ni kuhakikisha kuwa miradi yote iliyopokea pesa inatakiwa kukamilika ifikapo Desemba 30, 2024 ili Januari ianze kutoa huduma.
Aidha Mhe Kaminyoge amewataka mafundi wanaotekeleza miradi hiyo kuhakikisha wanaongeza vibarua na kuwalipa fedha kwa wakati ili miradi hiyo iende kwa kasi na kwa ubora unaotakiwa.
“Miundombinu ipatikane yenye ubora lakini wananchi waseme pesa aliyoleta Mhe Rais imewanufaisha wote” amesema Mkuu wa Wilaya
Kamati hiyo imetembela na kukagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kijiji cha Isageng’he Kata ya Sukuma, ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Mandang’ombe na Mbaragane Kata ya Mbaragane, ujenzi wa nyumba ya mwalimu (2 in1 ) katika shule ya sekondari Dakama.
Pia Kamati hiyo imekagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Mwabaraturu na ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Budekwa Kata ya Budekwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Julius John amesema kuwa upungufu wa wazabuni wanaoomba kazi kwenye mfumo wa NEST unaleta changamoto katika utekelezaji wa miradi kwa kuwa mpaka sasa mzabuni ni mmoja tu anayesambaza madini ujenzi.
Kaimu Mkurugenzi amesema Halmashauri imeendelea kutatua changamoto hiyo ili kuhakikisha utekelezaji wa ujenzi wa miradi hiyo unaendelea ili miradi hiyo ikamilike kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.