Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Maswa ikiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Maswa Ndg. Athuman Kalage akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Maswa pamoja na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wametembelea na kukagua miradi ya BOOST inayoendelea kujengwa katika Wilaya ya Maswa na kuwataka mafundi wote wanaotekeleza miradi hiyo wawe na mpango kazi wa kila siku ili kutoa taarifa kwa uongozi kwa ajili ya kushughulikia changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwa kuwa mpango kazi huo utasaidia mafundi hao kufanya kazi kwa weredi
Wakiwa katika ziara hiyo wamekagua miradi 5 ya BOOST inayotekelezwa ikiwepo Ujenzi wa shule mpya ya msingi yenye mikondo miwili iliyopo kijiji cha Igunya Kata ya Jija, Ujenzi wa shule mpya ya msingi yenye mkondo mmoja katika Kijiji cha Shishiyu Kata ya Shishiyu, Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo katika shule ya msingi Igunya iliyopo Kata ya Jija, Ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa ya mfano ya awali katika shule ya msingi Mwabayanda na Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo shule ya msingi Ngudu iliyoko Kata ya Bugarama.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.