Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Maswa imeridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Maswa hususani ujenzi wa shule mpya za sekondari na miradi mingine ya elimu na utawala
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh. Dkt Vincent Anney ameyasema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipokagua utekelezaji wa miradi hiyo leo tarehe 10 Machi 2025.
pia Mh. Dkt Anney ameipongeza Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo ambapo ameeleza kuwa changamoto ndogondogo ambazo zimejitokeza zifanyiwe kazi ili miradi ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Pia amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kuhakikisha wanaongeza kasi ili ifikapo April 30 2025 miradi hiyo iwe imekamilika.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kuhakikisha inatoa hati miliki kwa shule zote ili kuepusha migogoro baina ya taasisi na wananchi walio karibu na maeneo ya taasisi hizo.
kwa upande wao Wajumbe wa kamati hiyo wameipongeza Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi kwa kuwa kazi ni nzuri na pia wameiomba Halmashauri kutekeleza maelekezo yote ambayo Mwenyekiti wa Kamati hiyo ameyatoa ili fedha zilizotolewa zisiweze kurudi serikalini.
Katika ziara hiyo Kamati imekagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari Isagen’ghe iliyopo katika Kijiji cha Isageng’he Kata ya Sukuma , ujenzi wa jengo la ofisi ya utawala Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Pia wamekagua ujenzi wa shule mpya ya sekondari iliyopo kijiji cha Bukigi Kata ya Malampaka, mradi wa ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Badi pamoja na nyumba ya mtumishi katika shule ya sekondari Kulimimkuyuni iliyopo Kata ya Kulimi.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.