Wajumbe wa kamati ya fedha, utawala na mipango kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wameridhishwa na viongozi wanaosimamia miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa katika maeneo yao kwa kasi na ufasi mkubwa.
Akizungumza katika kijiji cha Mwabaraturu eneo ambalo shule mpya ya msingi inajengwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. Simon Berege ameipongeza kamati ya ujenzi kwa usimamizi mzuri wa mradi kwa kuwa shule hiyo inajengwa kwa ubora unaotakiwa na kasi yake ni nzuri.
Pia Mkurugenzi Mtendaji amemshauri msimamizi wa mradi kuwashirikisha kamati ya ujenzi katika manunuzi ya vifaa vinavyotumika kujenga mradi huo na si mtu mmoja kuchukua maamuzi ya kununua vifaa hivyo.
Mbali na shule hiyo wajumbe pia wametembelea kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini (CAMARTEC) kilichopo kijiji cha Mwandete Kata ya Sangamwalugesha na kuona zana mbalimbali ambazo zitasaidia katika shughuli za kuinua uchumi, mwananchi kwa kuwa zana hizo ni za technologia ya kisasa ikiwepo mashine ya kutengeneza siagi, mashine ya kupukuchua mahindi na nyingine nyingi.
Kamati imeishauri Divisheni ya Maendeleo ya Jamii kuona namna ya kuwawezesha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kupitia mikopo ya asilimia kumi kuchukua zana hizo ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuiwezesha Halmashauri kupata mapato kupitia miradi ambao watabuni.
Pia kamati imetembelea kikundi cha vijana imara kilichopo Kata ya Lalago kinachojishughulisha na mradi wa utengenezaji wa fensi waya (fence wire) ambacho kilipewa kiasi cha shs 16,000,000/= ambazo ni fedha za mikopo ya asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Wajumbe wamewashauri vijana hao kutoka na kujitangaza maeneo ya wazi ili wapate wateja na masoko kwa haraka ili waweze kupata fedha ambazo zitawasaidia kurudisha mkopo waliopewa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji amewapongeza vijana hao kwa kuanzisha kiwanda hicho ambacho kimeanza kufanya uzalishaji na amewaomba wawe na nidhamu katika matumizi ya fedha ili waweze kufika mbali pia ameahidi kuwapa eneo sehemu ya viwanda katika eneo la Ng’hami ili kuweka kiwanda chao.
Mwenyekiti wa Kamati amewataka vijana hao kuwa na ushirikiano katika kufanya kazi hiyo ili waweze kufikia malengo yao ya kukua katika biashara yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.