• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Kamati ya Fedha Utawala na Mipango yatembelea kiwanda cha Viatu Moshi

Posted on: July 22nd, 2022

Kamati ya Fedha Utawala na Mipango imefanya ziara ya kwenda kujifunza jinsi ya uendeshaji wa Viwanda katika Kiwanda cha Bidhaa za ngozi Kilimanjaro.

Katika ziara hiyo Kamati imekutana na Kamati Tendaji ya Manispaa ya Moshi kabla ya kutembelea kiwanda ambapo Mwenyeketi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mhe. Paul Simon Maige ametoa neno kuhusu lengo la safari ambalo lilikuwa ni kufika kujifunza na kupeana uzoefu juu ya usimamiaji na uendeshaji wa Viwanda. Akitoa neno la ukaribisho Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi  ameshukru kwa ujio na kukaribisha Wageni mjini Moshi. Ameeleza pia juu ya zawadi walizopata Maswa na walichojifunza wameishaanza utekelezaji ambapo wiki ijayo watafungua kampuni yao itakayosimamia masuala ya Viwanda katika eneo lao.

Akitoa taarifa ya Kiwanda Mkurugenzi wa Kiwanda ametoa historia fupi ya mradi kuwa ulianzishwa mwaka 1978 na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika eneo la Gereza la Karanga kwa ajili ya kutengeneza viatu. Mradi wa kiwanda cha bidhaa za Ngozi cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KLICL) unaendeshwa kwa ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Jeshi la Magereza kupitia kampuni yake ya Prison Corporation Sole (PCS).  Utekelezaji wa mradi huu unafanywa chini ya Kampuni ya ubia ijulikanayo Kilimanjaro International Leather Industries Co. Ltd (KLICL). Katika ubia huo Mfuko wa PSSSF unamiliki 86% ya hisa za Kampuni na Jeshi la Magereza linamiliki 14%.

Kampuni ya KLCIL inasimamia viwanda vya Kutengeneza Viatu, Soli, bidhaa za ngozi ( Ndala, mikanda, mabegi na pochi) na kuchakata ngozi. Ameshauri Wafugaji wafuge mifugo vyema kwa ubora ili ngozi za mifugo wao zipate soko. Akisisitiza amesema ngozi za mifugo wa kanda ya Ziwa na Nyanda za juu kusini zina ubora kwa hiyo ni nzuri kwa ajili kutengenezea viatu na bidhaa nyingine ukilinganisha na zinazopatikana katika kanda ya Kaskazini kutokana na hali ya hewa na malisho. Amesema ngozi za mbuzi ni nzuri kwa ajili ya kutengeneza viatu vya wanawake. Kwa msisitizo mkubwa amesema ili kampuni iweze kusimamia vema Viwanda Viongozi wake wanatakiwa wasiwe na mtazamo wa Kiserikali bali wanaojali kazi hii ndio inayowafanya wapate riziki ya kila siku.

Baada ya taarifa wenyeji walitupitisha sehemu mbalimbali kuona kazi zinazofanyika.

             Wajumbe wa Kamati ya FUM wakiwa safarini wakati wa ziara yao huko Moshi Kilimanjaro 22/07/2022

             Picha ya Pamoja ya Kamati ya FUM Maswa na CMT ya Manispaa ya Moshi 22/07/2022

  Mwenyekiti akisaini kitabu cha Wageni baadaya kukaribishwa kiwandani 

Mkurugenzi wa kiwanda cha bidhaa ya ngozi wa pili  kushoto akitoa taarifa fupi kwa Kamati ya FUM iliyotembelea kiwandani hapo 22/07/2022

Wajumbe wa Kamati ya FUM wakipokea taarifa kwa makini wakati Mkurugenzi wa Kiwanda akitoa taarifa 22/07/2022

Wajumbe wa FUM  wakipata maelezo wakati wa kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo

Wajumbe wa FUM wakiangalia baadhi ya bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo 22/07/2022


Matangazo

  • TANGAZO LA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI June 19, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WALIMU WA AWALI WAPATIWA MAFUNZO YA MBINU BORA ZA KUFUNDISHIA

    June 10, 2025
  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.