Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. Maisha Mtipa amewapongeza walimu wakuu pamoja na watendaji wa Kata kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Boost inayotekelezwa katika maeneo yao.
Ndg. Mtipa alisema hayo wakati wa ziara yake pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara walipotembelea miradi hiyo ili kuona hatua ilipofikia na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika ujenzi wa miradi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji pia amewapongeza mafundi wanaojenga miradi hiyo kwa kuwa kasi yao ni nzuri na pia wanajenga kwa ufanisi na weredi mkubwa pamoja na hilo amewataka waendelee kujenga vizuri kwa kuwa kuna miradi mingi inaendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa sababu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Elimu ikiwepo SEQUIP.
Akiwa katika ziara hiyo Ndg. Mtipa ametembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Nguliguli iliyopo Kata ya Nguliguli ambapo mradi huo upo katika hatua ya ukamilishaji na kiasi cha Fedha kilichotumika katika mradi huo ni shilingi milioni 56,000,000/=.
Pia alitembelea Shule ya Msingi Ipililo B iliyopo Kata ya Ipililo ambapo madarasa matatu yamejengwa na matundu matatu ya vyoo mradi huo unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 81,300,000/=.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji amefika katika ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ya mikondo miwili yenye madarasa 14 ya Shule ya Msingi na Madarasa mawili ya wanafunzi wa awali, matundu ya vyoo 24 na jengo moja la Utawala ambapo mradi huo upo katika hatua ya ukamilishaji na kiasi Cha Fedha kilichotumika katika mradi huo ni shilingi 540, 300,000/=.
Vileve mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika Shule ya Msingi Igunya Kata ya Jija mradi unatekelezwa na serikali kupitia mradi wa Boost ambapo kiasi cha shilingi 56,000,000/= zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Mkurugenzi Mtendaji pia alitembelea ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ya mkondo mmoja katika Kijiji Cha Shishiyu Kata ya Shishiyu wenye madarasa 7 ya shule ya msingi, madarasa 2 ya wanafunzi wa awali na matundu ya vyoo 16 na kiasi cha Fedha kinachotumika katika mradi huo ni shilingi 348,500,000/=.
Pia ziara hiyo ilifika mpaka Kijiji cha Mwakabeya Kata ya Ipililo ambapo ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ya mkondo mmoja inajengwa na serikali kupitia mradi wa BOOST kiasi cha shilingi 348,500,000/= zimetolewa ambapo mradi huo unaohusisha ujenzi wa madarasa 7 ya Shule ya Msingi, jengo la Utawala, madarasa mawili ya wanafunzi wa awali na matundu ya vyoo 16.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa inatekeleza miradi hiyo ambayo ilipata Fedha kutoka serikali kupitia mradi wa BOOST kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa shule mpya, madarasa na matundu ya vyoo na mpaka sasa miradi hiyo ipo katika hatua za ukamilishaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.