Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge ametoa maagizo kwa watendaji wa Kata, vijiji na Maafisa Tarafa kutatua kero na changamoto za wananchi kwa kufanya mikutano katika maeneo Yao ya kazi.
Mhe Kaminyoge ametoa maagizo hayo katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambacho kimehusisha watendaji wa Kata, vijiji, Maafisa Tarafa na wakuu wa idara.
Mkuu wa Wilaya amesema hayo ni maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Dkt Yahaya Nawanda kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa Halmashauri ya Wilaya, makatibu Tawala watendaji wa Kata na watendaji wa vijiji kuhakikisha wanasikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo Yao.
Mhe. Kaminyoge amesema kuwa ili kutatua kero za wananchi watendaji wa Kata, vijiji na Maafisa Tarafa wanatakiwa kuvua vyeo vyao ili wananchi wafike kwenye ofisi zao ambapo wananchi wanaamini shida zao zitatuliwa.
Pia amewataka watendaji hao kukaa ofisini kwa mujibu wa sheria ambazo ni kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la mwaka 1999 ambapo mtumishi anatakiwa kuwepo eneo la kazi kuanzia saa moja na nusu mpaka sasa tisa na nusu .
"Mkizingatia haya wananchi wakija wakawakuta kwenye ofisi zenu hatuwezi tukawa na malalamiko kero zingine zitaingia baadae kwa sababu wakati mwingine wananchi wanakuja mara tatu yaani siku tatu ofisi ya Mtendaji wa Kijiji imefungwa , ofisi ya Mtendaji wa Kata imefungwa anaamua kujopa rufaa mwenyewe kuja kwa mkuu wa Wilaya moja kwa moja." Mkuu wa Wilaya
Aidha ametoa maelekezo kwa watendaji wa Kata na vijiji kuanzia kesho waanze kufanya mikutano katika katika maeneo Yao kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi kwa kuzingatia ratiba ya kata husika ili kuniwezesha Mtendaji wa Kata kuhudhuriwa mikutano yote katika vijiji vyake.
Mkuu wa Wilaya ameongeza kuwa Mamlaka ya mji mdogo ipo kisheria hivyo amewataka viongozi wa maeneo hayo wakiwepo wenyeviti wa vitongoji kuhakikisha wanafanya mikutano ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwa kutoa majibu ya kero hizo.
Pia Mhe Kaminyoge amewataka watendaji kuitisha kamati ya maendeleo ya dharura kwa sababu ya kutoa maelekezo kwa wajumbe wote katika Kata kuanzia ngazi ya kitongoji wajue namna ya kutatua changamoto zinazojitokeza katika ngazi hizo kabla ya kufika kwa mtendaji wa Kata.
"Tukifanya hivi Yale malalamiko na kero ambazo zitakuwa zimewashida mzilete na sisi tukaja na kuzitoa kwa njia ya maandishi tuanamaliza kabisa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi kero nyingi kwa kweli zipo ndani ya uwezo wetu kwenye maeneo yetu tunayofanyia kazi."Amesema Mhe Kaminyoge
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.