• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

DC KAMINYOGE AZINDUA PROGRAMU JUMUISHI YA MALEZI, MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO

Posted on: March 1st, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Mhe. Aswege Kaminyoge amezindua program ya malezi , makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto yenye lengo la kukabiliana na kutokomeza changamoto ambazo ni kikwazo cha hatua sahihi za ukuaji timilifu wa mtoto kimwili, kiakili na kijamii kwa Watoto kuanzia umri wa miaka 0 hadi miaka 8

Ameyasema hayo katika uzinduzi wa program hiyo uliofanyika tarehe 28.02.2024 katika ofisi ya mkuu wa wilaya ambapo amesema ni maelekezo ya mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu kuwa program hiyo izinduliwe ngazi zote kuanzia taifa, mkoa hadi Halmashauri.

Amesema kuwa tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa umri wa miaka 0 hadi 8 ni umri nyeti wa kumtengeneza mtoto aliye dhaifu kimwili kiakili na kijamii kwa kuwa katika umri huo ubongo hupokea kile kinachoingia na kujengwa kutokana na kile anachokipata.

Ameongeza kuwa programu hiyo itatekelezwa kwa miaka 5 ambapo watoto wote wenye umri huo ili kukabiliana na kutokomeza changamoto zote ambazo ni kikwazo cha hatua sahihi na timilifu za ukuaji wa mtoto ambapo utekelezaji huo utahusisha wadau wote muhimu wa malezi makuzi matunzo ulinzi na maendeleo ya awali ya mtoto (MMMAM).

Aidha amesisitiza katika maeneo matano ambayo yanatakiwa kuzingatiwa wakati wa utekelezaji wa programu hiyo ambayo ni uzingatiaji wa huduma za lishe Bora kwa mtoto na mama, lishe ya kutosha kwa mtoto na mama mzazi kuanzia ujauzito.

Malezi yenye mwitikio, fursa za ujifunzaji wa awali na ulinzi na usalama kwa watoto ambapo programu hiyo ni mwitikio wa taifa katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya Dunia (SDGS)

Makusudi makubwa ya programu hii ni pamoja na kusaidia kuondokana na mmomonyoko wa maadiri unaochangia kutokea kwa vitendo vya ukatili ili kuijengea jamii uelewa na kuirudisha kwenye malezi salama kwa watoto amesema Mkuu wa Wilaya

Aidha amesema takwimu zinaonyesha kuwa robo tatu sawa na 66% ya watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 kusini mwa jangwa la Sahara wapo kwenye hatari ya kutokufika hatua timilifu za ukuaji kutokana na kukosa malezi Bora, umaskini, utapiamlo pamoja na matatizo mengine ya kijamii na kiuchumi.

"Nchini Tanzania 43% ya watoto (16, 694,763) wamefikia ukuaji timilifu ikiwa 57% wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu za ukuaji na maendeleo kutokana na viashiria ambapo watoto wa umri wa miaka 0 hadi 8 ni 30% ya watu wote." Ameeleza Mhe.  Kaminyoge

Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kuhakikisha idara zote zinazotekeleza programu hiyo kuhakikisha wanashirikiana na wadau kuelekeza na kusisitiza kuzingatia utekelezaji wa programu hiyo pamoja na kuandaa mipango kazi na kusaidia utengaji wa bajeti.

Amesisitiza  wakuu wa taasisi na wadau kupitia vitengo maalum vinavyosimamia ulinzi na usalama kuweka mipango kazi sambamba na wadau wa vituo vya malezi kuhakikisha vituo vyao vina vitendea kazi na vifaa vyote vya kujifunzia  kwa mtoto wa awali ili kuwawezesha watoto kuchangamshwa kimwili na kiakili.


Matangazo

  • TANGAZO LA UHAMASISHAJI CHANJO YA MIFUGO January 21, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MASWA

    March 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.