Balozi wa pamba Tanzania Mh. Agrey Mwanri amefanya ziara wilaya ya Maswa yenye lengo la kuelimisha wakulima wa pamba namna bora ya utumiaji wa viuwatilifu.
Akiwa kwenye ziara hiyo Mh Balozi ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, Katibu Tawala Wilaya pamoja na wataalamu kutoka Idara ya Kilimo.
Mh Mwanri ameelezea kuridhishwa na namna ambavyo baadhi ya wakulima wa pamba walivyofuata taratibu za ulimaji wa upana wa cm 60 kwa 30 na kutoa elimu ya vitendo kwenye mashamba hayo.
Aidha balozi amewasihi wakulima wa maswa kufatilia kwa karibu zao hilo maana linahitaji uangalizi ikiwepo upuliziaji wa dawa, palizi na kupunguzia pamba kwa wakati baada ya siku 21.
Kwa upande wake Afisa Tarafa ya Mwagala Ndg. James Hongoli akimwakilisha Mkuu wa Wilaya amesema serikali ya Mkoa wa Simiyu imejiwekea lengo la kupata tani laki tano za pamba kimkoa ( 500,000 ), tani laki moja na thelathini kiwilaya (130,000 ).
Vilevile mh Mwanri ametoa onyo Kali kwa wakulima ambao wanauza dawa za pamba mnadani hatua kali zitachukuliwa ikiwepo “kusukumwa ndani kama ambavyo imefanyika Igunga, Kishapu na Meatu” lengo likiwa ni kudhibiti upotevu wa viuwatilifu.
Kutoka na hayo yote baadhi ya wakulima wa pamba waliofikiwa na Mh. Balozi walipata fursa ya kutoa shukrani kwa elimu waliyoipata na wamewameahidi kufuata maelekezo yote yaliyotolewa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.