Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge amewapongeza viongozi wanaosimamia miradi ya maendeleo kwa kuwa miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili.
Kaminyoge amesema hayo Leo tarehe 30.06.2023 wakati akitembelea miradi hiyo katika Kata tatu za Wilaya ya Maswa.
Akiwa katika ziara hiyo Mhe mkuu wa Wilaya ametembelea ujenzi wa shule mpya ya msingi yenye mikondo miwili iliyopo Kijiji Cha Igunya Kata ya Jija ambapo ujenzi wake upo katika hatua ya kupaua, mradi huo unatekelezwa kwa kiasi Cha shilingi milioni 540,300,000/= kutoka serikali kupitia mradi wa boost.
Pia amekagua ukarabati wa shule kongwe ya msingi Malampaka ambapo Serikali imetoa kiasi Cha Shilingi milioni 180,000,000/= kwa ajili ya kukarabati shule hiyo ambayo ujenzi wake upo katika hatua ya umaliziaji. Ujenzi wa shule mpya katika Kata ya Shishiyu mradi ambao unatekelelezwa na serikali kupitia mradi wa boost ambapo kiasi Cha shilingi milioni 348,500,000/= zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Vilevile DC Kaminyoge amekagua mradi wa ujenzi wa majengo ya OPD, Maabara, chumba Cha kujifungulia kina mama ( maternity), chumba Cha upasuaji( theatre) na kichomea taka katika kituo Cha afya Shishiyu, mradi huo unatekelezwa na serikali kupitia Fedha za Tozo ambapo kiasi Cha shilingi milioni 500,000,000/= zimetolewa ili kukamilisha mradi huo ulio katika hatua ya ukamilishaji kwa asilimia 98.7%.
Aidha mkuu wa wilaya amewasisitiza mafundi kuzingatia muda waliopewa wa kukamilisha mradi ili kuwawezesha watoto katika maeneo hayo kupata Elimu katika shule hizo pamoja na wananchi kupata huduma za afya katika kituo hicho cha Shishiyu.
Katika wilaya ya Maswa mradi wa boost unatekeleza miradi ya ujenzi wa shule mpya 3, madarasa ya mfano 2, vyumba vya madarasa 38 na matundu ya vyoo 65.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.