Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh. Dkt Vincent Anney tarehe 07 Machi, 2025 amepata fursa ya kujitambulisha na kuzungumza na Watumishi wa Wilaya ya Maswa katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya amewataka watumishi wa Wilaya ya Maswa kuwa wabunifu katika kazi zao na maisha yao binafsi pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mapato katika vyanzo walivyonavyo na kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitaisaidia kuongeza mapato katika Wilaya ya Maswa.
Pia Mh.Dkt Anney amewataka Wakuu wa Idara na viongozi wa ngazi zote kuhakikisha wanashirikiana kikamilifu katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ili ikamilike kwa wakati ambapo amesisitiza ifikapo Aprili 30, 2025 miradi yote inayotekelezwa iwe imekamilika.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa mamlaka ya mji mdogo Maswa kusimamia usafi wa mazingira kwa kuhakikisha wanaweka mfumo mzuri wa ukusanyaji wa taka na kuandaa dampo la taka ambapo taka zote zitatupwa hapo ili mji wa Maswa uwe safi.
Sambamba na hilo pia amewataka watumishi wote kuhakikisha wanawahi kazini na kujiepusha na utoro ili waweze kuwatumikia wananchi kwa weredi.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.