• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

DAS Maswa ataka ajenda ya lishe iwe muhimu katika vikao

Posted on: August 23rd, 2023

Katibu Tawala wa Wilaya ya Maswa Ndg. Athuman Kalage amewataka wakuu wa Divisheni zote zinazohusika na masuala ya lishe wahakikishe kuwa katika vikao vyao ajenda ya lishe iwe ya kudumu na waandae mpango kazi ambao utawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi katika kutekeleza shughuli zote za lishe Bora kwa kuwa wao ndio wanabeba ajenda hiyo.

Katibu Tawala alisema hayo katika kikao cha Kamati ya  lishe Wilaya kilichofanyika katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa chenye lengo la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2023 ambapo Divisheni zinazohusika na utekelezaji wa afua hizo ziliwasilisha taarifa zao.

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya elimu ya awali na Elimu msingi Dkt. Lucy Kulong'wa alisema kuwa Divisheni hiyo ilipewa kiasi cha shilingi Milioni 3 na Laki Tisa  kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe katika shule 135 za Msingi katika Wilaya ya Maswa lengo ni kuhakikisha shule zote zinatoa chakula kwa wanafunzi shuleni na kutekeleza shughuli mbalimbali ikiwepo utoaji wa Elimu katika shule zote 135, kupanda miti ya matunda pamoja na mbogamboga.


"Tumefanikiwa kutoa Elimu kwa walimu pamoja na maafisa Elimu Kata juu ya uhamasishaji na utoaji wa Elimu ya utoaji wa chakula mashuleni, tumefanikiwa kwa 95% ya shule 135 zinatoa chakula pamoja na uji mashuleni." Amesema Dkt Lucy.

Pia ameongeza kuwa upatikanaji wa  huduma ya chakula mashuleni utasaidia ufaulu wa wanafunzi kuongezeka.

Afisa lishe wa Wilaya ya Maswa Ndg. Abel Gyunda amewataka maafisa Elimu wa Wilaya kuwasisitiza walimu wakuu na wakuu wa shule kupeleka mahindi yao katika mashine yenye virutubishi vya lishe ambapo lengo likiwa wanafunzi hao wapate chakula chenye virutubishi vya aina nne ambavyo vitawasaidia kupata mlo kamili utakaowasaidia  kufikili vizuri na kufanya vizuri katika masomo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Ndg. Robert Urassa alisema katika utekelezaji wa afua za lishe Divisheni hiyo imehamasisha wakulima katika vikundi vya  vijana na wanawake juu ya umuhimu wa ulaji wa mahindi lishe, viazi lishe, matumizi ya mbogamboga, sambamba na kuendesha mafunzo ya usindikaji wa mahindi kwa kuweka virutubishi kwenye unga wa mahindi (fortification) .

Aidha Ndg Urassa amesisitiza kuwa Divisheni imetoa Elimu juu ya unywaji wa maziwa kwa kuadhimisha siku ya maziwa duniani katika shule 10 za msingi ambapo wanafunzi wamepewa Elimu ya umuhimu wa maziwa mwilini na kuwashauri watumie glasi moja ya maziwa kila siku pamoja na kula vyakula vyenye lishe bora.

Mratibu wa lishe Divisheni ya Elimu Sekondari Ndg. Mathayo Maingu alisema mpango wa lishe katika shule za Sekondari ulilenga kuanzisha Bustani za mbogamboga na matunda lengo likiwa ni kuongeza thamani ya chakula kwa wanafunzi  ambapo shule zote zilipata Elimu hiyo ambayo iliongozwa na Afisa Lishe wa Waliya kwa kuhamasisha uanzishaji wa Bustani hizo na kuanzisha klabu za lishe ambazo zitasaidia kuendelea kuhamasisha ufanyikaji wa shughuli za utunzaji wa Bustani hizo ambapo shule 16 zimefanikiwa kuanzisha Bustani za mbogamboga na zingine kushindwa kutokana na changamoto ya ukame.

Nae Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Basila Bruno alisema Divisheni yao imetekeleza afua za lishe kwa kutoa Elimu kuhamasisha wananchi kula vyakula vyenye virutubishi vyote vyenye kuhusisha makundi yote matano ya lishe ambapo Elimu ya lishe bora imetolewa kwa wananchi 1878 wanaume 1020 na wanawake 858 katika Kata zote 36 kwa akina mama wajawazito, watoto, akina mama wanaonyonyesha, wazazi na walezi pamoja na wanafunzi katika shule tofautitofauti.


Matangazo

  • TANGAZO LA UHAMASISHAJI CHANJO YA MIFUGO January 21, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MASWA

    March 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.