Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Maswa.
Timu ya Menejimenti imekagua miradi hiyo tarehe 06 Desemba, 2024 na kutoa ushauri kwa wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha wanasimamia kwa weredi miradi na kutoa taarifa mapema pindi wanapopata changamoto katika utekelezaji wa miradi hiyo ili changamoto hizo ziweze kutatatuliwa.
Katibu wa Kamati hiyo ambaye pia ni Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg, Masanja Kengese ametoa wito kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili wakamilishe miradi hiyo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili ifikapo mwezi wa kwanza miradi hiyo ianze kutumika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakandarasi hao wanaotekeleza miradi hiyo wameiomba timu ya menejimenti kuwahimiza wazabuni wanaosambaza madini ujenzi kuhakikisha wanafikisha madini ujenzi hayo katika maeneo husika ya ujenzi ili kuwarahisishia mafundi kufanya kazi kwa urahisi ili waweze kukamilisha kazi kwa muda uliopangwa.
Timu ya menejimenti imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya Afisa Ugani katika Kata ya Sengwa yenye thamani ya shs milioni 38, ujenzi wa shule mpya ya sekondari Mwabaraturu iliyopo Kata ya Mwabaraturu yenye thamani ya shilingi milioni 584.
Aidha timu imekagua mradi wa vyumba 3 vya madarasa na matunda 6 ya vyoo katika shule ya msingi Budekwa iliyopo Kata ya Budekwa yenye thamani ya shilingi milioni 88, ambapo ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji.
Pia wajumbe wa timu hiyo wamekagua Ujenzi wa nyumba ya walimu (2in1) shule ya sekondari Dakama yenye thamani ya shilingi milioni 100, ujezi wa nyumba hiyo upo katika hatua ya msingi, ujenzi wa jengo la Zahanati Kijiji cha Mbaragane Kata ya Mbaragane lenye thamani ya shilingi milioni 92.
Pamoja na ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika kata ya Sukuma yenye thamani ya shilingi milioni 584 ambapo ujenzi wake upo katika hatua ya msingi.
PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA ZIARA YA CMT KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MASWA
Timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Maswa ikikagua ujenzi wa nyumba ya Afisa Ugani katika Kata ya Seng’wa katika ziara yao ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi tarehe 06 Desemba 2024.
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ikikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 3 na matundu ya vyoo 6 katika shule ya Msingi Budekwa iliyopo Kata ya Budekwa katika ziara yao ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi tarehe 06 Desemba 2024.
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ikikagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Mwabaraturu ikiwa ni ziara yao ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi, tarehe 06 Desemba 2024.
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ikikagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu (2 in 1) katika shule ya Sekondari Dakama iliyopo Kata ya Dakama ikiwa ni ziara yao ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi tarehe 06 Desemba 2024.
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ikikagua ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Mbaragane kilichopo Kata ya Mbaragane katika ziara yao ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi tarehe 06 Desemba 2024.
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ikikagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari katika Kata ya Sukuma ikiwa ni ziara yao ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi, tarehe 06 Desemba 2024.
Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ikikagua ujenzi wa Ofisi ya Utawala katika Kitongoji cha Ng’hami Kata ya Nyalikungu ikiwa ni ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi, tarehe 06 Desemba 2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.