Kamati ya Menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu imefanya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Halmashauri hiyo na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ambayo imefikia hatua nzuri ya ukamirishaji.
Wajumbe hao wamewaomba viongozi waliopewa jukumu hilo la kusimamia miradi hiyo wahakikishe miradi inakamilika kwa muda uliopangwa na iwe na ubora wenye viwango vinavyotakiwa ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Wakiwa katika ziara hiyo wajumbe wa kamati ya CMT wamekagua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa katika shule ya sekondari Zanzui iliyopo Kata ya Zanzui Halmashauri ya Wilaya ya Maswa. Fedha zilizotumika katika utekelezaji wa mradi huo ni Jumla ya shs 50,000,000/= zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Maswa mpaka sasa mradi huo umetumia shs 49,646,389/= ambapo mradi huo umekamilika kwa asilimia 90%.
Pia kamati ya CMT imetembelea mradi wa ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Zawa kilichopo Kata ya Mwang’honoli, mradi unaotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kutumia mapato ya ndani ambapo Kijiji cha Zawa kimepokea shs 53,765,534.74 za awamu ya pili ya ukamilishaji wa zahanati hiyo mpaka sasa jumla ya shs 11,448,137 zimetumika katika mradi huo.
Mradi huo wa zahanati ukikamilika utasaidia wananchi wa eneo hilo kutotembea umbali mrefu kufuata huduma, itapunguza vifo vinavyotokana na uzazi kwa kuwa huduma itakuwa karibu.
Mradi wa nyumba ya mtumishi katika Kijiji cha Kizungu Kata ya Buchambi mradi huo unatekelezwa na serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kiasi cha shs 62,262,102.00 kimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba hiyo ambayo ipo katika hatua ya boma kiasi kilichotumika mpaka sasa ni shs 16,087.500.00 mpaka sasa pia mradi huo una miezi mitatu(3) tangu kuanza na unatarajiwa kukamilika juni 2023.
Kwa upande wao viongozi hao wameahidi kufanya kazi ya kusimamia kwa karibu miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kusaidia jamii inayozunguka maeneo hayo kupata huduma hizo za kijamii na kuhakikisha sehemu ambapo kuna mapungufu watahakikisha wanarekebisha.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.