Wataalamu kutoka Wilaya za Mkoa wa Simiyu wameingia siku ya pili leo katika mafunzo ya kuanza kutumia mfumo wa IMIS ( Insurance Management Information System) unaotekeleza CHF iliyoboreshwa. Mfumo huu unalenga kukusanya taarifa za wanachama kutoka ngazi ya kijiji kwa kutumia wanajamii wenyewe. Mafunzo haya katika Mkoa yamegawanyika katika makundi mawili, la kwanza linajumuisha Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi na Busega, kundi la pili linajumuisha halmashauri za Itilima, Maswa na Meatu. Kila Halmshauri imetoa washiriki 10 ambao wanapata maelekezo kisha wakatoe elimu kwa washiriki watakao toka ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya na waandikishaji watakao toka ngazi za vijiji au mitaa.
Katika mafunzo haya pia mfumo wa JAZIA - PVS ambao unasaidia upatikanaji wa dawa pale zinapokosekana katika bohari ya taifa ya dawa (MSD) umeelekezwa na utekelezaji wa DHFF kwa kutumia mfumo wa kutolea taarifa za kifedha kwenye vituo vya kutolea huduma (FFARS).
Wanachama wa CHF iliboreshwa watakuwa na faida ya kutibiwa mahali popote hapa nchini kwa kutumia kadi zao za uanachama ambapo awali walikuwa wanatibiwa kwenye kituo walipo sajiliwa tu. Huu mfumo hadi sasa Mikoa mitatu imeishaanza kuutekeleza na umeonyesha mafanikio makubwa.
Mafunzo haya yanaendeshwa na wakufunzi kutoka Mkoani, TAMISEMI na wadau kutoka HPSS.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.