• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Mrejesho |
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Divisheni
      • Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Miundombinu, Maendeleo ya Vijijini ya Mjini
      • Kilimo, Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Uratibu
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Tehama
      • Huduma za Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Usimamizi wa Ununuzi
      • Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira
      • Mawasiliano Serikalini
      • Usimamizi wa Taka na Usafi
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Sheria ndogo
    • Fomu
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

Bilioni 3.1 kujenga miundombinu ya Shule Maswa

Posted on: July 3rd, 2023

Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ni miongoni mwa Halmashauri zilizonufaika na Fedha kutoka SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili za sekondari katika Kata ya Kulimi, Kata ya dakama na ujenzi wa nyumba za walimu aina ya two in one katika shule ya sekondari Mashimba na Shule ya sekondari Nyongo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge leo tarehe 03.07.2023 wakati akiendelea na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kupitia mradi wa Boost katika Tarafa ya Mwagala

Mkuu wa Wilaya amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea Fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kulimi ambayo mradi wa ujenzi huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 584, ujenzi wa shule mpya katika Kata ya Dakama ambayo nayo imepewa kiasi Cha shilingi milioni 584, ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shule ya Sekondari Mashimba na Shule ya Sekondarii Nyongo ambazo kila nyumba itagharimu kiasi Cha shilingi milioni 100 Fedha ambazo zimetolewa na serikali kupitia mradi wa Secondary Education Quality Improvement Program (SEQUIP).

Mhe. Kaminyoge ametoa wito kwa wataalamu kutoa Elimu kwa kamati za ujenzi ili waweze kuelewa majukumu yao na kuepusha migogoro katika utekelezaji wa miradi hiyo.

Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya amekagua ujenzi wa Soko katika mji wa Maswa awamu ya pili ambalo lipo katika hatua ya ukamilishaji, Fedha zilizotumika katika mradi huo ni shilingi milioni 55 ambazo zimetolewa na mfuko wa Jimbo. Ujenzi wa shule mpya ya msingi iliyopo Kijiji cha Mwakabeya Kata ya Ipililo yenye mkondo mmoja wenye madarasa 9, matundu ya vyoo 16 pamoja na jengo la Utawala moja jumla ya shilingi milioni 348,500,000/= zimetolewa na serikali kupitia mradi wa BOOST kutekeleza mradi huo.

Aidha ametembelea ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Ipililo “B” mradi huo unatekelezwa na BOOST ambapo kiasi Cha shilingi milioni 81,300,000/= kimetolewa, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule  ya Msingi Nguliguli wenye thamani ya Shilingi 56,300,000/= ambapo miradi yote ipo katika hatua ya ukamilishaji.

Akizungumza kwa nyakati tofauti mkuu wa wilaya amesisitiza kamati ya ujenzi kushirikiana na mafundi kwa karibu ili kuwezesha miradi kukamilika kwa wakati, pamoja na  kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Mhe. Kaminyoge amemwagiza Mhandisi wa Wilaya kupanua Soko kuu la Maswa  ili liweze kuwa na vizimba 30 ambavyo vitawawezesha wafanyabiashara 30 kutumia Soko hilo ambalo kwa sasa lina vizimba 20 ambayo havitoshelezi mahitaji ya wafanyabiashara hao.

Ujenzi wa madarasa

Ujenzi wa Soko


Matangazo

  • TANGAZO LA UHAMASISHAJI CHANJO YA MIFUGO January 21, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI May 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI May 27, 2022
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO May 30, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA NeST KWA WATAALAMU WA UNUNUZI WILAYANI MASWA

    March 27, 2025
  • DKT ANNEY; NENDENI MKASIMAMIE MIRADI YETU VIZURI

    March 26, 2025
  • VIKUNDI 15 VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU VYAPATA MKOPO

    March 26, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAPONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO MASWA

    March 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Fursa za uwekezaji Mkoani Simiyu
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Sensa ya mwaka 2022
  • Taarifa ya Mapato na matumizi
  • Mfumo wa FFARS
  • Mfumo wa IMIS
  • Mfumo wa PlanRep
  • Government Web Framework
  • Mfumo wa PREM
  • Maswa DC Mail Domain
  • Hotuba ya Mh. Waziri Mkuu PLANREP/FFARS

Viunganishi linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Simiyu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • TAMISEMI
  • Sekretariet ya Ajira
  • Ikulu
  • Baraza la Mitihani Tanzani
  • Wizara ya Elimu Tanzania
  • Wizara ya Afya
  • Wizara ya Fedha
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana Nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

    Sanduku la Posta: 170, MASWA

    simu ya Mkononi: +255 282 750 271

    Simu: +255 282 750 271

    Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.