Baraza la wafanyakazi Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu limepitisha Rasimu ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya shilingi bilioni 52.4 kwa mwaka wa fedha wa 2024/2025 ambapo limetoa mapendekezo katika maeneo ya kimkakati kutengewa bajetu ili kuongeza tija katika ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Hayo yamesemwa leo katika kikako cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.
Awali akiwasilisha bajeti hiyo afisa mipango na uratibu Ndg Steven Musika amesema katika utekelezaji wa mpango na bajeti ya maendeleo wa mwaka 2024/2025 Halmashauri imekadiria kukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni 52.4 ikiwa ni ongezeko la shilingi milioni 6.5 sawa na asilimia 14%.
Ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2023/2024. Ya kiasi cha shilingi bilioni 45.9 ambapo ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa fedha za mishahara ya ajira mpya na upandishaji vyeo kwa watumish.i
Aidha amesema katika mapendekezo ya mpango na bajeti yamezingatia vipaumbele katika maeneo muhimu ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwa kujenga madaras 64, maabara 6, utengenezaji wa madawati 750, viti na meza 180 na ujenzi wa matundu ya vyoo 227.
Kuimalisha ukusanyaji wa mapato ambapo shilingi milioni 100 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika minada mikubwa ya Shanwa na Senani, kujenga kitega Uchumi katika eneo la MADECO, uanzishwaji wa karakana ya matengenezo ya magari pamoja
kuimarisha miundombinu ya afya kama vile ukamilishaji wa zahanati 4, ujenzi wa matundu ya vyoo 15 katika Zahanati 5na ukamilishaji wa vituo vya Afya 3 ili kuboresha huduma za Afya kwa kuhakikisha viyuo vya kutolea huduma vilivyopo vinapata dawa na vifaa tiba kwa ajili ya wagonjwa.
pia upatikanaji wa pembejeo za kilimo na mifugo, upimaji wa afya ya udongo masoko ya mazao sambamba na kuendeleza kilimo cha umwagiliaji chenye tija , kupanda miti milioni 2 ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuimarisha usafi na hifadhi ya mazingira.
“Halmashauri imetenga jumla ya shilingi milioni 191 kwa ajili ya kuboresha hali ya lishe wilayani ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza na utapiamlo sambamba na hilo pia imetenga shilingi milioni 327 kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa fursa ya mikopo nafuu ya asilimia 10% kwa shughuli za ujasiliamali.” Amesema Afisa mipango na uratibu
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Bw. Maisha Mtipa amewataka Wakuu wa Divisheni kuboresha mambo yote yaliyoshauriwa ili yaonekane katika bajeti zao.
Pia ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuongeza bajeti ya watumishi kutoka shilingi bilioni 24 ambayo Halmashauri ilitenga hadi kufikia shilingi bilionoi 26. Amesema
“Mhe Rais ameongeza zaidi ya bilioni mbili katika bajeti yetu kwa hiyo serikali yetu sasa hivi inajali watumishi zamani ilikuwa unatenga bilioni 24 lakini unaweza kupata bilioni 20 tunampongeza Mhe. Rais kwa kuwa anajali watumishi.” Mkurugenzi Mtendaji
“Niwaombe tu watumishi sisi ni watumishi wote tukafanye kazi kwenye maeneo yetu na tukawe wawakilishi wa wenzetu katika haya mambo kwa sababu sisi tunawawakilisha watu wengi kule waliopo, tukawaeleze miradi tunayotekeleza, iliyopo na sisi ni wasimamizi wa miradi hii tukaisimamie kwa uaminifu mkubwa.” Amesema Bw. Mtipa
Ameongeza kuwa walimu wana miradi ya madarasa na watumishi wa afya wana miradi ya zahanati hivyo amewataka kusimamia kwa uaminifuili ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Maswa na amewahasa kufanya kwa kuzingatia sheria na taratibu
Watumishi wana haki ya msingi lakini haki haiwezi kuja bila kutekeleza wajibu, kwahiyo wajibu tuufanye ibaki mwajiri au menejimenti iweze kukupa haki yako kwa hiyo tukatekeleze kwa mujibu na tukawaambie wenzetu wakatekeleze wajibu wao katika maeneo ya kazi na changamoto zote tumezichukua kutazifanyia kazi.mkurugenzi mtendaji
Pia Mkurugenzi Mtendaji amewataka watumishi kuhakikisha wanahamasisha suala la ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao ili yaweze kusaidia katika masuala mbalimbali pamoja na kueleza miradi yote inayotekelezwa kwa mapato ya ndani.
Kwa upande wao wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wameshauri maeneo yote ya kimkakati yapewe kipaumbele ikiwepo maeneo ya skimu za umwagiliaji majosho, pamoja na Barabara ili kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanaongezeka.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.