Balozi wa pamba Tanzania Mhe. Agrrey Mwanri amefanya ziara katika wilaya ya Maswa yenye lengo la kutoa mafunzo ya namna bora ya matumizi ya viuatilifu kwa kuwasisitiza wakulima wa pamba kuhakikisha wanafuatilia pamba yao kwa Kila hatua ikiwa wao wenyewe ni mabibi shamba na mabwana shamba hivyo jukumu la kuiangalia pamba ni la mkulima mwenyewe pamoja na kuhakikisha wanapulizia kwa wakati kabla ya wadudu kuingia katika zao hilo.
Pia amewaagiza viongozi wote wa AMCOS kutoa viuatilifu na mabomba kwa wakulima wote waliopata mafunzo kwa vitendo na kwa wale wote ambao wamechanganya pamba na mazao mengine na walioacha maotea hawatapata viuatilifu na mabomba ikiwa ni makubaliano ya wakulima wote katika mkutano wa kijiji wameazimia katika mkutano huo kuwa yeyote aliyeotesha maotea hatapata vinyuvyizi na viuatilifu.
Kwa upande wake Afisa Tarafa wa Tarafa ya Mwagala Ndg. James Hongoli amesema watasimamia kwa karibu viuatilifu vyote na mabomba ambayo yatatolewa na bodi ya pamba pamoja na serikali ili kuzuia wizi na kuwachukulia hatua wale wote waliopalilia masalia.
Nae Diwani wa Kata ya Mpindo Mhe. Amos Ntabo amemshukuru sana Mhe. balozi wa pamba Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya tangu namna ya kuandaa shamba mpaka namna ya kunyunyizia na ameahidi watazingatia maelekezo yote waliyopata kwenye mafunzo na wameahidi kuwa mabalozi wazuri kwa wengine ambao hawakufika katika mafunzo hayo.
Wakulima wa pamba wamemshukuru balozi wa pamba kwa kuwapa Elimu hiyo ambayo itawasaidia kuongeza tija na uzalishaji katika zao hilo na kuongeza mapato yao na wilaya kwa ujumla.
Akiwa wilaya ya Maswa balozi wa pamba ametembelea kata nne na vijiji 8 kutoa Elimu ya kutosha kuhusu namna bora ya unyunyuziaji, namna ya kutumia viuatilifu na namna ya kuchanganya dawa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.