Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Maswa Mashariki na Jimbo la Maswa Magharibi Ndg. Maisha S. Mtipa leo tarehe 25 Agosti 2024 amekutana na viongozi wa vyama vya siasa ambapo amewataka kwenda kutoa elimu na hamasa kwa wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo linatarajiwa kuanza tarehe 4-10 Septemba 2024.
"Tumewaita hapa mkatoe hamasa, elimu juu ya uandikishaji ili watu wajitokeze kwa kiasi kikubwa ili wakajiandikishe katika maeneo yao maana mtu asipojiandikisha katika kipindi hiki cha uboreshaji yawezekana akakosa haki ya kupiga kura." ameeleza Afisa Mwandikishaji
Pia Ndg Mtipa amesema zoezi hilo litawahusu watu wote waliofikia umri wa miaka 18 na kuendelea na wale watakaotimiza umri huo ifikapo uchaguzi mkuu wa 2025, kutoa kadi mpya kwa wale waliopoteza au kuharibika na wale ambao wamekosa sifa ya kuwemo kwenye daftari kutokana na kifo.
Pia Afisa Uchaguzi ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha wanawasilisha orodha ya mawakala yenye barua za utambulisho pamoja na picha na kwa wale ambao hawana picha wawe na nakala ya kitambulisho cha nida au kitambulisho chochote kinachotambulika.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.