Wednesday 29th, January 2025
@Jihu - Lalago
Mwenge wa uhuru Wilayani Maswa utapokelewa kutoka Wilaya ya Kwimba tarehe 22/5/2019 na kukimbizwa katika vijiji vyake.
Shamrashamra za mapokezi zitakuwa katika kijiji cha Jihu kata ya Badi.
Mwenge utafungua miradi mbalimbali ya maendeleo, kukagua shughuli za vikundi mbalimbali katika vijiji vya kata za Badi, Malampaka, Isanga, Nyalikungu, Sukuma na Lalago.
Vijiji vitakavyopitiwa na Mwenge ni kama ifuatavyo: Jihu, Mhida, Ikungu, Nyashimba 'S', Bukigi, Malampaka, Bukangilija, Nhelela, Njiapanda, Isulilo, Busamuda, Sayusayu, Nyanguganwa, Binza, Nyalikungu, Shanwa, Sola, Mwadila, Hinduki 'M', Mbaragane, Mandang'ombe na Lalago.
Mkesha utafanyika katika eneo la Lalago mjini.
Wananchi wote mnakaribishwa kushangilia katika maeneo yenu na katika mkesha mjini Lalago.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.