Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Aswege Kaminyoge anawakaribisha wananchi wote wa Wilaya ya Maswa kuja kushiriki katika shamrashamra za kuupokea Mwenge wa Uhuru, kuukimbiza katika maeneo mbalimbali Wilayani hapa wakati ukipita kukagua, kutembelea, kuona, kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya Mandeleo siku ya Tarehe 26/7/2023.
Shamrashamra za Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2023 zitafanyika katika Kijiji cha Sangamwalugesha Kata ya Sangamwalugesha kuanzia saa 12.00 asubuhi na Mkesha utakuwa katika Kijiji cha Malampaka Kata ya Malampaka. Karibu tuushangilie, tuupokee, tuukimbize na tusherehekee pamoja.
Mwenge utapita katika Kata zifuatazo;
Sangamwalugesha, Lalago, Mbaragane, Sukuma, Ng’wigwa, Nguliguli, Zanzui, Sola, Nyalikungu, Shanwa, Binza, Buchambi, Busangi, Isanga, Badi, Malampaka na Masela
“Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa”
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.