Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary T. Mugumba amefanya ziara katika Wilaya ya Maswa leo tarehe 7/3/2019 ambapo ametembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Kinamwigulu, Shamba la pamba la kikundi cha Wanawake ch Upendo.
Katika skimu ya umwagiliaji kinamwigulu ameweza kupata taarifa na changamoto kutoka kwa wananchi wanaonufaika na mradi huo. Wananchi wameomba lijengwe bwawa ili kilimo cha umwagiliaji kiweze kufanyika muda wote kwa mwaka.
Mhandisi wa umwagiliaji tume ya kanda ya ziwa ya umwagiliaji ameahidi kuja kufanya tathmini kwa kupima hali na ikolojia ya eneo hilo kuona kama panafaaa ili lichimbwe bwawa. Aidha ameitaka Halmashauri kupanga bajeti kwa Miradi kama hii ili kuikwamua katika hali iliyofikiwa. Sambamba na hili amewashauri wananchi wanufaika wa mradi huu watoe michango yao ili kuwezesha ukamilishaji wa mradi kwa ajili ya manufaa yao.
Katika shamba la Pamba la kikundi cha upendo cha akina mama kijiji cha Busamuda amepokea risala iliyopongeza juhudi za serikali ya awamu ya Tano inayowajali wananchi wake. Kikundi hicho kimelima ekari 5 za Pamba baada ya kupata Mkopo wa Tsh.750,000/= kwa ajili Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Kutia kikundi hicho Diwani wa Kata ya Busangi Mhe. Paul Nyondwa Njige ameshukuru juhudi za Serikali ya awamu ya Tano kwa kutoa mikopo kwa Wanawake iliyosababisha akina mama wa kikundi cha Upendo kunufaika.
Baada ya kukagua miradi hiyo amefanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Isulilo. Ameongelea suala la kilimo cha Pamba alivyoona katika maeneo aliyopita na shamba alilotembelea la kikundi cha wanawake cha upendo ilivyo nzuri. Pia suala la viuatilifu inaonekana havitoshi ila serikali ina utaratibu wa kuongeza.
Mwisho amewasisitiza wananchi kulima kwa kutumia mbolea ili kuongeza mavuno ya mazao ya chakula na biashara.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.