Waziri wa maji Jumaa Aweso amewapongeza viongozi wa jeshi la Sungusungu kwa kutengeneza jeshi ambalo lipo tayari kuwa mstari wa mbele kulinda amani na Usalama wa Taifa la Tanzania .
Ameeleza kuwa jeshi hilo ni la mfano na linatakiwa kuigwa kwa kuwa linafanya kazi pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza majukumu ya ulinzi na Usalama wa Taifa.
Mhe Aweso amesema hayo wakati akizungumza na jeshi hilo la sungusungu katika Kata ya Seng’wa Wilayani Maswa.
Pia Mhe Aweso ametoa pongezi kwa Sungusungu kwa kuonyesha moyo wa kizalendo ujasiri kwa ajili ya kulilinda Taifa katika ngazi hiyo ya chini .
"Ulinzi wa Taifa letu unaanzia kwa wananchi wenyewe wakiwemo wanasungusungu mmeonyesha uzalendo mmeonyesha utayari, mmeonyesha ujasiri wa kulilinda Taifa letu lakini pia kumlinda Rais wetu." Ameeleza Mhe. Aweso
Pia Waziri Aweso amechangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya kuliunga mkono jeshi hilo kwa kazi kubwa inayofanyika ya kulinda amani na usalama.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.