Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dr. Frederick Damas Sagamiko amegawa vitambulisho vya matibabu bure kwa wazee 51 katika kijiji cha Mwabagalu Kata ya Nyabubinza Wilayani hapa.
Akiongea na Wazee hao amewashukuru kwa kujenga Taifa letu na kusema ni jukumu la Serikali kuhakikisha Wazee wanalindwa na kutibiwa bure. Amewaomba wazee hao kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata matibabu pale wanapokuwa wanaumwa bila bughudha yoyote.
Kupitia kusanyiko hilo Afisa Ustawi wa jamii ndugu Abacos D. Kululetela amesema zoezi hili ni endelevu kwa Wilaya nzima kuwa wazee wote wanapata vitambulisho vya matibabu bure.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.