Watendaji wa Kata 3 za Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wamekabidhiwa pikipiki kwa lengo la kuongeza kasi ya ukusayaji wa mapato usimamizi wa miradi ya maendeleo na kuongeza uwajibikaji kwa kutatua kero mbalimbali wananchi.
Akizungumza katika zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge amesema pikipiki hizo zikatumike kuwahudumia wananchi katika kutatua changamoto na kero mbalimbali pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
Pikipiki hizo zimetolewa na Wizara ya TAMISEMI kwa watendaji wa Kata za Mwabayanda, Shishiyu na Bugarama ikiwa ni mwendelezo wa serikali kusogeza huduma kwa wananchi.
Pia Mhe. Kaminyoge amesisitiza kuwa vyombo hivyo visitumike kwa shughuli binafsi za kiuchumi bali vitumike kuleta manufaa kwa wananchi.
“Chombo hiki ni cha umma mnatakiwa msaidiane na watendaji wa vijiji ambao hawana pikipiki kwa maana yake muende kuelimisha wakulima tumieni chombo hiki pamoja msiwe na ubinafsi.” ameeleza Mkuu wa Wilaya
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.