Wananchi wa kitongoji cha Ng'hami Kata ya Nyalikungu Wilayani Maswa wamekuwa na mkutano dhidi ya kupata taarifa ya ujenzi wa Viwanda katika eneo la Viwanda la Ng'hami (Ng'hami Industrial Zone).
Timu ya Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imefika katika eneo hilo kutoa taarifa ya juu ya neema na fursa zinazolifikia eneo la Ng'hami.
Mkutano umefanyika katika eneo la shule ya Msingi Ng'hami kuanzia saa 8.30 alasiri.
Viwanda vinavyotarajiwa kuanza ujenzi hivi karibuni ni Kiwanda cha chaki na Kiwanda cha vifungashio.
Wananchi wamehaswa pia kuchangamkia fursa zinazokuja hivi karibuni katika eneo lao.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.