Pamba ni nyuzi nyeupe na laini zinazotokana na tunda la mpamba, upekee huu wa pamba umeisukuma wto shirikisho la biashara duniani kutenga siku maalum ya kuadhimisha na kuonyesha namna ambavyo zao hilo linagusa maisha ya wananchi ya kila siku katika kujikimu. Zaidi ya aslimia 40 ya Watanzania hutegemea zao la pamba kiuchumi.
Tafiti zinaonyesha kuwa zao la pamba linashambuliwa na wadudu aina ya funza wa vitumba, chawajani, kalidea n.k ambao wakiachwa bila kudhibitiwa husababisha hasara zaidi ya mavuno yote.
Katika nchi ya tanzania mikoa 17 inalima zao hilo la pamba ikiwemo Simiyu mikakati madhubuti imechukuliwa na serilkali kupitia Bodi ya Pamba Tanzania kuhakikisha kuwa zao hilo linakuwa salama na linaleta tija kwa wakulima.
Bodi ya Pamba Tanzania kupitia kwa Balozi wake Mh. Agrey Mwanri imeanzisha “campaign” maalum ya kuhamasisha wakulima na kutoa elimu ya namna bora ya kupulizia pamba ili kudhibiti wadudu hao ambao wamekuwa tishio kwa wakulima.
Akiwa mkoani Simiyu wilaya ya Maswa Mh. Mwanri ametembelea kata nane (8) na vijiji kumi na tano (15) kuelimisha wakulima wa pamba jinsi ya kupulizia na kuchanganya dawa kwa kufuata taratibu ili kunusuru zao hilo lisiendelee kuathirika.
Mh. Balozi amewataka wakulima hao kutumia viwatilishi ambavyo vinatolewa na amcos ambavyo ni Tegata, Mo strong, Cynofos 550plus ec na Eakil 13sc kupulizia katika mashamba yao ili pamba zao zisishambuliwe na wadudu.
Kwa upande wake Mkuu Wa Wilaya ya Maswa Mh. Aswege Kaminyoge amempongeza Mh. Balozi kwa kutoa elimu hiyo kwa wakulima wa Maswa na kuwaagiza watendaji wote kuanzia ngazi ya kijiji, kata, maafisa ugani na watendaji wote wa serikali kusimamia kwa ukaribu zao hilo kwa kuendelea kuwaelimisha wakulima jinsi ya kupulizia dawa, ufatiliaji wa palizi na kupunguzia mimea kwenye mashamba. Lengo likiwa ni mkulima katika wilaya ya Maswa kuzalisha pamba kwa tija ili aweze kupata kuanzia kilo 600 mpaka 2500 kwa heka ili kukuza uchumi na kuwahakikishia wakulima kuwa viwatilifu vitaanza kugawiwa pamoja na pampu.
Pia wakulima wamemshukuru Balozi wa pamba kwa elimu aliyoitoa na wameahidi kuitumia vizuri na kupongeza technologia mpya ambayo wamejifunza ya kutumia pampu mpakato yenye uwezo wa kunyunyuzia heka nne tofauti na ile ya lita 16 ambayo ilikuwa inachukua muda mrefu.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.