Viongozi wa vyama vya ushirika (AMCOS) Wilayani Maswa wamekaa kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa lengo la Maandalizi ya kufanikisha malengo yao musimu huu wa mwaka 2019.
Mkurugenzi Mtendaji amewakumbusha kuepuka changamoto walizokutana nazo musimu uliopita ili kwa kipindi hiki wafanye vizuri zaidi. Amewashauri wajifunze changamoto walizopata wakati wa kugawa mbegu za Pamba kwa Wakulima zikawe chachu ya wao kugawa viuwatilifu bila tatizo lolote.
Aidha katika kikao hicho wamekubaliana kuanza kufanya biashara ya ununuzi wa mazao mchanganyiko kwenye maeneo yao. Hili linafanyika ili kuokoa upotevu wa ushuru wa mazao mchanganyiko unaotokea kila mwaka.
Ili kufanikisha shughuli za maendeleo Wilayani Maswa, ushuru unatakiwa ukusanywe vizuri, hivyo vyama vya msingi kwa kila kijiji vimekubaliana na hili kuepusha upotevu wa makusanyo hayo. Kwa kupitia ununuzi wa mazao mchanganyiko itakuwa ni mwanzo wa maandalizi ya ununuzi wa zao la Pamba mwaka huu.
Viongozi hao wamekubaliana na kuahidi kwenda kujiandaa kwa kazi hii kwani musimu wa mazao mchanganyiko umeanza sasa.
Kwa pamoja , ushirikiano na uaminifu tunaweza kuinua uchumi wa Maswa.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.