Vijana wa Kike chini ya Mradi wa Vijana tunaweza unaofadhiliwa na shirika la UNFPA na kutekelezwa na Restless Development wamekutana na Viongozi wa serikali Wilayani Maswa leo tarehe 24/09/2021.
Mradi wa Vijana Tunaweza ni mradi wa kuwezesha wasichana unaotekelezwa na Restless Development wenye lengo la kupunguza visababishi vinavyopelekea wasichana kuingia kwenye maambukizi ya VVU na UKIMWI, mimba zisizo tarajiwa ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni. Vijana tunaweza hutumia mbinu shirikishi ambayo inapambania elimu ya makuzi, haki na afya ya uzazi uwezeshaji wa kiuchumi na kuwajengea kujiamini katika kufanya maamuzi yanayogusa maisha yao.
Ndani ya Wilaya ya Maswa mradi huu ulianza mwaka 2021 mwezi 3 na unawafikia mabinti wenye uzao mmoja 30 wakiwa wameunganishwa kwenye vikundi vidogo 3 ndani ya kata ya Lalago, Badi na Sola hapa Wilaya ya Maswa. Katika kufanikisha utekelezaji wa mradi huu, shughuli mojawapo ni vijana kukutana na viongozi wa Serikali na wadau wengine mbalimbali ambao wanamchango mkubwa katika kufanikisha maendeleo ya vijana na kuwasilisha maoni na mapendekezo, kujadiliana nao katika ufumbuzi wa changamoto mbalimbali na kutengeneza mahusiano mazuri na endelevu.
Kati ya Mambo yaliyojadiliwa na vijana wa Kike Kutoka Katika Kata ya Badi, Sola na Lalago ni pamoja na :-
Kaimu Mkurugenzi katika kuhitimisha aliwahakikishia vijana kuwa kupitia katika vikundi vyao watapata mikopo ya kisheria itolewayo na Halmashauri kwa Vijana , Wanawake na Watu wenye ulemavu, pia aliwaagiza watendaji wote walio chini yake kuhakikisha wanasikiliza kero za Vijana wa kike na kuzitatua pindi zitokeapo ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha katika vikao ili watoe maoni na mapendekezo yao.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji aliwashukuru sana Viongozi wote walioanzisha Mradi huu wa Vijana tunaweza kwa nia yao njema ya kuwajengea vijana wa kike uwezo wa kujiamini na kuwainua kiuchumi.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.