Sekta ya Elimu ni nyenzo muhimu sana katika maisha ya kila mtanzania kwa kuliona hilo divisheni za Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa zimewapima uelewa wanafunzi katika wiki ya maadhimisho ya sherehe za miaka 61 ya uhuru wilayani Maswa ambapo shule mbalimbali za msingi na sekondari zimejitokeza kuandika insha kuhusiana na mafanikio ambayo serikali imepata katika sekta ya Elimu tangu uhuru hadi leo.
Leo tarehe 7 Decemba 2022 mashindano ya kuandika insha yamefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Nyalikungu na kuhusisha shule za sekondari Binza, Nyalikungu, Mwakaleka pamoja na Maswa kwa upande wa shule za msingi zilizoshiriki ni Ng'hami, Shanwa na Mwawayi.
Katika mashindano hayo shule zilizofanya vizuri zaidi kila kundi ni kama ifuatavyo; kwa upande wa Shule za Sekondari ni Mwakaleka na kwa upande wa Shule za msingi ni Nyalikungu.
Akizungumza katika eneo hilo la ukumbi wa Nyalikungu Afisa Elimu vifaa na takwimu Ndg. Aloyce Emmanuel Mtayoba amesema kuwa wameamua kuwapima watoto hao wa shule ili kuona uelewa wao kuhusu mafanikio ambayo serikali imepata tangu uhuru mpaka sasa, katika sekta ya Elimu.
Pia amesema kuwa katika maadhimisho hayo Divisheni za Elimu Msingi na Sekondari zimeziagiza shule zote kuchukua miti Halmashauri na kwenda kupanda miti katika shule zao na michezo mbalimbali iendelee pamoja na mazoezi ya kuandika insha mpaka siku ya kilele Cha maadhimisho hayo yatakayofanyika tarehe 9.
Wanafunzi wa Shule za Sekondari wakiandika Insha siku ya tarehe 7/12/2022
Wanafunzi wa Shule za Msingi wakiandika Insha siku ya tarehe 7/12/2022
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.