Leo tarehe 12/3/2018 kulikuwa kikao cha Wadau wa elimu Wilayani Maswa ambacho Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka. Kikao hicho kimejumuisha Waheshimiwa Madiwani, Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule, Maafisa Elimu Kata, Wenyeviti wa Kamati za Shule, Wakuu wa Idara na Walimu.Katika kikao hicho Mgeni rasmi ametoa zawadi za majiko ya gesi kwa shule 20 zilizofanya vizuri kwenye mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi darasa la saba Mwaka 2017, ametoa vyeti kwa Wadau mbalimbali wanaochangia shughuli za maendeleo ya Elimu, ametoa vyeti kwa shule 10 zilizofanya vizuri mtihani wa Mock na shule 10 zilizofanya vibaya mtihani wa Mock. Amepokea na kugawa magunia ya mahindi kwa shule za Msingi za Wilaya ya Maswa yaliyotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kuchangia chakula cha Wanafunzi shuleni. Aidha amefungua mashine za kutolea nakala aina ya RISO zitakazotumiwa kwa ajili ya kudurufu mitihani na kazi mbalimbali za kitaaluma ili kusaidia kupunguza garama za uendeshaji wa Shule Wilayani Maswa.
Sambamba na utoaji zawadi ametoa hotuba juu ya manufaa ya elimu kwa jamii ili kuleta mapinduzi ya maendeleo. Amesema ilikuwa na maendeleo katika eneo lako lazima elimu iwe kipaumbele katika eneo hilo, kwa kusisitiza amese "tazama nchi zilizoendelea ndizo zina Vyuo bora, na hata miji iliyoendelea ndiyo ina vyuo bora". Katika hili Wazazi na Walezi wamehimizwa kusomesha watoto wao ili kuandaa misingi mizuri kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya ya Maswa. Ili kukabiliana na mabadiliko ya Sayansi na teknolojia kia mzazi au mlezi ajiandae kumuelimisha mwanaye.
Kuhusu suala la chakula amehaidi kwa kushirikiana na Afisa Elimu wa Mkoa atakutana na Wenyeviti wa Kamati za shule ili wakahamasishe wazazi kuchangia chakula ili watoto wasome vizuri.
Aidha amewataka wazazi kuwasimamia watoto wao ili wasome na siyo kutoa lawama kwa walimu na hali matatizo yanaanzia kwenye familia. Hii itasaidia kila mtu kusimamia majukumu yake ya kuendeleza suala zima la elimu. Kila Mzazi au Mlezi ahakikishe mtoto ananidhamu anaenda shule na Mwalimu ahakikishe anafundisha wanafunzi.
Amewahasa wazazi na walezi wanaowakataza watoto kwenda shule au kufanya vibaya mitihani yao ya mwisho kutoendelea na tabia hiyo mbaya maana inarudisha maendeleo nyuma.
Ametoa maamuzi kuwa wanafunzi wote wa kidato cha sita Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 3/4/2018 hadi 17/4/ 2018 watakuwa kwenye makambi ya kujifunzia. Wasichana watakuwa shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na Wavulana watakuwa Shule ya Sekondari Binza.
Amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji kuwapa zawadi watumishi waliofanya vizuri majukumu yao na kuleta tija kwa jamii na taasisi yao siku ya maadhimisho ya mei mosi
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.