Leo katika sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge Mkoani Geita Mgeni rasmi wa sherehe hizo, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mhungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa kupitia hotuba yake ameagiza mikoa yote inayoongoza kwa utoro wa wanafunzi shuleni wadau wa elimu mikoani humo wasimamie kwa karibu suala la kudhibiti utoro.
Amewakumbusha wananchi kuwa elimu ni ufunguo wa maisha hivyo kila mzazi hana budi kuwekeza katika elimu kwa watoto wao.
Ametaja Mikoa iliyokithiri kwa utoro hapa nchini ambayo ni pamoja na Tabora 9.7%, Geita 8.1%, Mtwara 6.1% na Shinyanga 6.3% kwa Elimu Sekondari na Mikoa ya Rukwa 3.2%, Geita 3.1%, Tabora 2.9%, Singida 2% na Simiyu 2% kwa Elimu Msingi. Tathmini ya ujumla inaoonyesha shule za Sekondari zinaongoza kwa asilimia kubwa ya suala la utoro wa wanafunzi. Amesisitiza kwa kusema "Nitumie nafasi hii kuikumbusha Mikoa yote niliyoitaja hapa, kuwahamasisha wananchi wakiwemo wazazi, walezi na wanafunzi wenyewe kuhusu umhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni kwa kutumia taratibu za sheria tulizojiwekea katika maeneo yetu".
Hili limeambatana na Kauli mbiu ya Mwenge mwaka huu 2018 isemayo "Elimu ni ufunguo wa Maisha , wekeza sasa"
Kila mdau wa elimu anatakiwa ahusike sehemu yake ili kuinua kiwango cha elimu kitakachopelekea kuleta maendeleo katika jamii inayotuzunguka.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.