Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Kenani Labani Kihongosi ametoa wito kwa wananchi wa Maswa Mkoani Simiyu kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa litakalofanyika 27 Novemba 2024
Mhe Kihongosi amewaomba wananchi kuchagua viongozi Bora na sio Bora kiongozi wenye sifa, uwezo na maarifa, ambao watashirikiana na serikali kupeleka maendeleo katika kijiji, kitongoji na Kata husika katika eneo hilo.
"Ukijipima ukaona una uwezo nenda kavute fomu gombea mwenyewe na kama mnaona kuna watu wazuri Wana uwezo, Wana dhamira ya dhati ya kutumikia wananchi wapeni nafasi Waende kuongoza." Amesema Mkuu wa Mkoa
Mhe Kihongosi amesema hayo wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Kata za Mpindo Senani Ipililo na Nguliguli zilizopo Wilayani Maswa Mkoani Simiyu Leo tarehe 27 septemba 2024.
Kauli mbiu "Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi Tujitokeze Kushiriki Uchaguzi"
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.