Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenani Kihongosi ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kupata hati Safi iliyotolewa na mthibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG.
"Niwapongeze Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa hati Safi zipo baadhi ya Halmashauri zina hati ya mashaka wengine Wana hati chafu lakini katika Halmashauri ya Maswa, mkuu wa Wilaya hongereni mambo yenu hapa ni mazuri."
Aidha Mhe kihongosi amesema kikao hicho ni mwendelezo wa maagizo ya Mhe Rais na waziri wa TAMISEMI kwa wakuu wa mikoa kukaa na kujadili hoja zote zipatiwe ufumbuzi ili Halmashauri iendelee kuwa Bora.
"Niombe wanaohusika na hoja timizeni kwa Mamlaka zenu waweze kuchukuliwa hatua kwa sababu Kuna hoja zingine ni kwa uzembe wa makusudi na Kuna hoja ambazo sio za uzembe wa makusudi mtazame namna gani mtaweza kuchukua hatua ili serikali izidi kuaminiwa na wananchi ili kazi iendelee kufanyika."
Mkuu wa Mkoa ametoa pongezi hizo katika kikao cha kusikiliza repoti ya mthibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa tarehe 20 Juni 2024.
Katika kikao hicho Mhe kihongosi amesisitiza ukusanyaji wa mapato ambapo amemuomba Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha wanafikisha asilimia 100 ifikapo mwisho wa mwaka huu wa Fedha kwa kuwa ana timu nzuri ya wataalamu ili kufikia lengo ambalo waliokubaliana katika Baraza la madiwani.
Sanjali na hilo Mkuu wa Mkoa awevitaka vikundi vyote ambayo vilichukua mikopo ya asilimia 10 na havijarejesha Fedha hizo kurejesha mara moja vinginevyo hatua Kari za kisheria zitachukuliwa juu yao
"Fedha za vikundi zirudi waliokopeshwa wameshatumia wazilete tuwape vijana wengine waende kutumia Fedha za serikali kwa sababu kama mtu amekopa anashindwa kurejesha maana yake huyu mtu anawamyima fursa watanzania wengine ambao wangeweza kutumia Fedha hizo." Rc kihongosi
Pia Mkuu wa Mkoa ametoa ushauri na nasaha kwa viongozi na watumishi wa Maswa "Ninawaomba sana upendo ndio ukawe nguzo kuu katika utendaji wetu wa kazi, maandiko yanasema palipo na upendo ndio Pana Kila kitu pendaneni, saidianeni, shirikianeni ili muisaidie nchi yetu."
Akitoa taarifa katika kikao hicho Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. CPA Lwiza amesema hoja zilizotolewa na mthibiti na Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka 2022/2023 zilikuwa hoja 128 ambapo menejimenti imetoa majibu ya hoja zote ndani ya siku 21 kama Sheria ya ukaguzi NA 11 ya mwaka 2018.
Katika majibu hayo menejimenti imefanikiwa kutekeleza hoja 113 na kubaki na hoja 15 ambazo zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.