Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenani Kihongosi ametoa pongezi kwa watumishi wa Maswa kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika wilaya hiyo.
Mhe Kihongosi ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo aliyoifanya katika Wilaya ya Maswa
“Watumishi wa Maswa hongereni sana mzidi kutoa ushirikiano kwa Mkurugenzi wenu, Mkuu wa Wilaya na vyombo vyote vilivyopo hapa, kila mmoja ana wajibu wa kuitumikia nchi hii tumepewa vipande, tumepewa dhamana, tumepewa kazi na tuliomba kazi na Mungu akatujalia tukapata kazi, wajibu wetu kila mmoja akawajibike ajue ana deni.”
Pia amewataka watumishi hao kutendea kazi dhamana walizopewa kwa kuwatumikia wananchi ambao wanalipa kodi na fedha hizo zinatumika katika utekelezaji wa miradi hivyo amewaomba watumishi hao kuwajibu katika usimamizi wa miradi hiyo kwa weredi.
Akiwa Wilayani Maswa Mkuu wa Mkoa amekagua ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya sekondari Mwagala iliyopo kata ya Lalago ambapo Serikali kuu imetoa kiasi cha shs milioni 156 na mradi huo upo katika hatua ya ukamilishaji.
Pia amekagua mradi wa ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita laki mbili na mfumo wa usambazaji maji katika vijiji vya Zanzui, Malita na Mwabujiku wenye thamani ya shs bilioni 1.5, ujenzi wa kiwanda cha mtu binafsi cha kuchakata pamba kilichopo eneo la Nghami Kata ya Nyalikungu wnye thamani ya shs bilioni 1.5.
Aidha mkuu wa mkoa amekagua ujenziwa majengo yamionzi,maabara, kichomea taka na wodi binafsi pamoja na ukarabati wa mfumo wa umeme katika hospitali ya maswa yenye thamani ya shs milioni 900 fedha kutoka serikali kuu ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa mita 850 kutoka posta hadi njiapanda (Ikulu Road).
Pamoja na mradi wa kiwanda cha kufyatua tofari cha kikundi cha vijana wa Upendo Shanwa kilichopata mkopo wa shs. Milioni 9.4 kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kilichopo katika eneo la viwanda Ng’hami Kata ya Nyalikungu.
Miradi hiyo ikikamilika itataua changamoto mbalimbali katika wilaya ya maswa zikiwepo za ajira, afya elimu na usafirishaji.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.