Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Dkt Yahaya Nawanda amempongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwawezesha wanawake wa mkoa wa simiyu
Amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika leo tarehe 08 march 2024 katika viwanja vya Dutwa vyilivyopo kata ya Dutwa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu ambapo maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya “wekeza kwa mwanamke kuharakisha maendelo ya Taifa na ustawi wa jamii”
Amesema kuwa katika kuhakikisha anamtua ndoo mama kichwani Rais ametoa kiasi cha shilingi bilioni 444 kwa lengo la kuhakikisha wakina mama wote wa Mkoa wa Simiyu hasahasa wa Wilaya ya Busega, Bariadi na Itilima wanapata maji ya kutosha kwa awamu hiyo ya kwanza ya mradi.
“Mhe Rais licha ya kutuletea hizo fedha Zaidi ya bilioni 444 pia mhe rais katika bajeti hii kuhakikisha wanawake wote wa Mkoa wa Simiyu wanapata maji na tunapeleka maji kwa Zaidi ya asilimia 85% ifikapo mwakani.”amesema Mkuu wa Mkoa
Ameongeza kuwa Rais ametoa Zaidi ya shilingi bilioni 31 kuhakikisha miradi 32 inapelekwa katika Wilaya zote ili kuhakikisha mwanamke anatuliwa ndoo kichwani
Amesema maadhamisho hayo ni kumbukumbu ya mkutano uliofanyika Ubeligiji mwaka 1995 ambapo mkutano huo uliazimia kuwepo na usawa katika jamii, kupinga vita ya ubaguzi pamoja na ubakaji na uzalilishaji kwa wanawake na watoto.
Aidha amesema maadhimisho yaho ni kuenzi maadhamisho yaliyokuwa yameasisiwa kule Ubeligiji ambapo Mkoa wa Simiyu umeendelea kupinga vikari ukatili wa kijinsia katika nafasi mbalimbali na hasahasa kuhakikisha wanawake wanaendelea kuishi katika mazingira salama.
Amesisitiza kuwa mwanamke akiwa mbele jamii itaendelea kuwa mbele na kuwa salama Zaidi pia kauli mbiu hiyo itumiwe katika Mkoa wa Simiyu ili kuwawezesha wanawake kujiunga katika vikundi mbalimbali ambapo Zaidi ya wanawake 1527 wamejiunga katika vikundi 840 katika Mkoa wa Simiyu na tayari wameanza kupata mikopo ya asilimia 10% katika Halmashauri zote.
“Mhe Rais katika Mkoa wetu wa Simiyu ametutaka Mkoa wa Simiyu kutenga bajeti katika mwaka 2023/2024 Zaidi ya shilingi milioni 816 ili kupeleka katika vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu asilimia 10% yetu ya mapato ya Halmashauri tupeleke katika vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu.”amesema Dtk Nawanda
Pia ameongeza kuwa Mkoa wa Simiyu umekusanya milioni 500 katika asilimia 10% kwa ajili kwa ajili ya kukopesha wananwake, vijana pamoja na watu wenye ulemavu ambapo wamepanga kuwakopesha wananawe Zaidi ya bilioni 220 na tayari utaratibu umefika.
Dkt Nawanda ametoa wito kwa vijana kuiga mfano kwa akina mama pindi ambapo wanakopeshwa waweze kurudisha kwa wakati sambamba na hilo amewaagiza Wakurugenzi kuendelea kutenga fedha za asilimia 10% ili kuweza kufikia vikundi vingi vya akina mama.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.