Mkuu wa Divisheni ya kilimo ufugaji na uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa amewapongeza wananchi wa Kijiji Cha Mandang'ombe kwa mwitikio mkubwa waliouonyesha katika uzinduzi wa ugawaji wa nyandarua kwa Kila kaya ambapo lengo ni kutokomeza malaria katika kaya zao
Amezungumza hayo leo tarehe 07 march 2024 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji wa vyandarua wakati akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge katika kijiji Cha Mandang'ombe Kata ya Mbaragane
Ndg Urassa amesema wilaya ya Maswa miongoni mwa Halmashauri tatu za Mkoa wa Simiyu zenye kiwango Cha juu Cha maambukizi ya malaria kwa asilimia 21.8% hii ni kutokana na takwimu za utafiti wa afya na viashiria vya malaria vya mwaka 2022( TDHSIMIS).
Ameongeza kuwa kiwango hicho Cha maambukizi kimesababishwa na mvua nyingi zinazoendelea kumyesha, mito pamoja na shughuli za kilimo Cha mpunga na ufugaji vimesababisha mazalia mengi ya mbu kwa kipindi kirefu.
Pia ameishukuru serikali kupitia wizara ya afya , mpango wa taifa wa kudhibiti malaria kwa kushirikiana na ofisi ya Rais TAMISEMI na wadau wa mradi wa tvca
"Nichukue fursa hii kuwapongeza sana wananchi wa maswa kwa kujitokeza kwa wingi kuweza kuandikishwa ili kuweza kupata vyandarua hivi." amesema Ndg Urassa
Pia Wilaya inaendelea na mapambano dhidi ya malaria ambapo kiwango cha maambukizi ya malaria kimeongezeka kutoka asilimia 5% mwaka 2017 mpaka kufikia asilimia 28 ili kupunguza maambukizi ya malaria katika maeneo ya wananchi yenye kiwango kikubwa cha maambukizi
Wilaya itagawa vyandarua vyenye viutilifu ambapo vyandarua 295839 katika Kata 36 Vijiji 120 na Vitongoji 510 sawa na Kaya 73547 sawa na wananchi 554476 watanufaika kwa mujibu wa takwimu za usajili wa kaya uliofanuika februari 2024.
"Kila mmoja wenu kwa nafasi yake ahakikishe vyandarua vitakavyogawiwa vinatunzwa na vinatumika kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya malaria na si matumizi mengine kama alivyoongea Diwani na Mwenyekiti wa kijiji ameongea juu ya umuhimu wa kutumia vyandarua hivi."
Na mimi nisisitize wanacnhi wote mtakaopata vyandarua hivi mvitumie kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo kwa kuwa matumizi yasiyo sahihi yanarudisha nyuma lengo la serikali la kupunguza maambukizi ya malaria.
Aidha amesisitiza wanachi kuendelea kutumia afua zingine za kinga na tiba ikiwepo kuweka mazingira safi na kuzuia maji kutwama na kufukia madibwi ili kuweza kudhibiti maambukizi ya malaria sambamba na hilo ametoa wito kwa watendaji wa kata, vijiji na wananchi kuhakikisha wanafukia madimbi ili kutokomeza mazaria ya mbu kwenye kaya zao
Vilevile amesema serikali inayoongozwa na Dkt Samia imehakikisha vituo vya kutolea hudumaza afya za umma vinakuwa na vitenganishi kwa ajili ya uchunguzi wa marlaria na dawa zinatolewa bila malipo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Mbaragane Ndg Nkinda Masele ameishukuru serikali kwa kuwasaidia wananchi kupata neti ili kupambana na malaria kwa kuwa Tanzania bila malaria inawezekana.
Pia amewataka wananchi kunitumia neti hizo vizuri na si vinginevyo na pia ametoa wito kwa yeyote atakayeitumia neti vibaya yupo tayari kumchukulia hatua kwa sababu anavunja utaratibu wa Chama na serikali .
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.