Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mhe. Paul Maige amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasan kwa kuwapatia pikipiki 9 kwa ajili ya kukusanya mapato na kupeleka huduma kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi pikipiki hizo katika uwanja wa ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Leo tarehe 02 march 2023 Mhe. Maige amesema pikipiki hizo zitumike kukusanya mapato na kulinda kila aina ya mapato ambayo yatapatikana pembezoni mwa Wilaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndg. Simon Berege amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kuwapa pikipiki hizo ambazo zitatumika kwa shughuli za kiserikali, maendeleo na kukusanya mapato.
Amesisitiza kuwa pikipiki zilizotolewa kwa awamu hii watapewa watendaji wa pembezoni mwa Wilaya ya Maswa na awamu itakayofata watendaji wa maeneo mengine watapata pikipiki hizo.
Nae mwakilishi wa watendaji wa Kata Ndg. Paul Masaga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kuwapatia vitendea kazi hivyo pia ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kuzingatia umbali anapofanyia kazi mtendaji kuja makao makuu na ameiomba serikali iendelee kutoa vitendea kazi hivyo kwa watendaji wote.
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Sangamwalugesha Ndg. Modesta Ndelu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hasan, Mkuu wa Wilaya ya Maswa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa kumuwezesha usafiri maana anapoishi ni umbali wa km 68 kufika makao makuu ya Wilaya hivyo ujio wa pikipiki hiyo utakuwa mwarobaini katika kutimiza majukumu yake na ameahidi kufanya kazi kwa ufanisi kwa ajili ya kukusanya mapato na kuhudumia wananchi.
Katika kuboresha maslai na vitendea kazi hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imetoa pikipiki hizo kwa watendaji wa kata walio pembezoni mwa wilaya ambapo kata zilizonufaika ni Senani, Sangamwalugesha, Mpindo, Nyabubinza, Mwabaraturu, Seng'wa, Masela, Jija na Ipililo.
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Sanduku la Posta: 170, MASWA
simu ya Mkononi: +255 282 750 271
Simu: +255 282 750 271
Barua Pepe: ded@maswadc.go.tz
Copyright ©2022 Maswa District Council. All rights reserved.